JE! NI KWELI KUWA KRISTO ALIFUFUKA SIKU YA PASAKA KULINGANA NA MAANDIKO?

  Maswali ya Biblia, Uncategorized

SWALI: Naomba kuuliza, Je! Ni kweli kuwa Kristo alifufuka siku ya pasaka kulingana na maandiko matakatifu?


JIBU: Jibu ni hapana, biblia inasema Kristo alifufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma na sio siku ya pasaka. Pasaka na siku ya kufufuka kwa Bwana ni vitu viwili tofauti.

Marko 16:9 NAYE ALIPOFUFUKA ALFAJIRI SIKU YA KWANZA YA JUMA, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. 

Tofauti na watu wengi leo hii walivyofundishwa, wanavyofundishwa, na kudhani kuwa, siku ya pasaka na siku ya kufufuka kwa Kristo ni kitu kimoja, jambo ambalo si sahihi hata kidogo, siku ya kufufuka kwa Kristo na siku pasaka ni siku mbili tofauti, na wala Kristo hakufufuka siku ya pasaka, badala yake ni kuwa, Bwana na wanafunzi wake walijinja na kuila pasaka usiku ule (sawasawa na sheria ya Musa), kabla ya Yeye kwenda kusurubiwa.

Luka 22:8 Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, MKATUANDALIE PASAKA TUPATE KUILA

9 Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? 

10 Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingie katika nyumba atakayoingia yeye. 

11 Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki wapi chumba cha wageni, NIPATE KULA PASAKA HUMO pamoja na wanafunzi wangu? 

12 Naye atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo. 

13 Wakaenda, wakaona kama alivyowaambia, wakaiandaa pasaka. 

14 Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. 

15 Akawaambia, Nimetamani sana KUILA PASAKA HII pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; 

Na wakati walipokuwa wakila, ndipo Kristo alipoiingilia pasaka hiyo (ya sheria ya Musa), kwa kutoa mkate na divai (kuashiria mwili wake na damu yake kwa ajili ya ukombozi), 

Matayo 26:26 Nao WALIPOKUWA WAKILA YESU ALITWAA MKATE, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; HUU NDIO MWILI WANGU

27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Nyweni nyote katika hiki; 

28 kwa maana hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. 

Na kuanzia hapo sikukuu hiyo ya kusherekea pasaka kwa Wakristo Sawasawa na sheria ya musa ili ishia hapo (yaani kula mikate isiyotiwa amira n,k), kwa sababu Kristo ni mwisho wa hiyo sheria na Ndiye Pasaka Wetu. 

1 Wakorinto 5:7 Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana PASAKA WETU amekwisha kutolewa kuwa sadaka, YAANIKRISTO

Na pale tunapoumega mkate na kushiriki kikombe, hapo ndipo tunapoiadhimisha pasaka yetu, na si kula mikate isiyo na amira au kuchinja Mwana Kondoo n,k (hivyo vilikuwa vikimfunua Kristo). Na ndio sababu ya mtume Paulo kusema hivi juu ya SIKUKUU hizo za kiyahudi ikiwepo na Pasaka.

Wakolosai 2:16  Basi, mtu ASIWAHUKUMU ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa SABABU YA SIKUKUU au mwandamo wa mwezi, au sabato; 

17 mambo hayo NI KIVULI CHA MAMBO YAJAYOBALI MWILI NI WA KRISTO

Hivyo kwa kuhitimisha ni kuwa, Kristo hakufufuka siku ya pasaka kulingana na biblia, bali ni alfajiri siku ya kwanza ya juma.

Bwana akubariki, Shalom.

Tafadhari washirikishe na wengine habari hii njema.

+255652274252/ +255789001312


Mada zinginezo:

NAONA KUNA SINTOFAHAMU KUHUSU KRISMASI, HIVI NI KWELI IPO KWENYE MAANDIKO?


MCHUNGAJI WAKO NI NANI?


MAKANISA NA MAFUNDISHO YA UONGO YANAYOPOTOSHA WATU WENGI NYAKATI HIZI ZA MWISHO (sehemu ya 10)


NIKAWAONA WAFU, WAKUBWA KWA WADOGO, WAMESIMAMA MBELE YA KITI CHA ENZI.


JE! NI KWELI KUWA MAANDIKO MATAKATIFU NI JUMLA YA VITABU 66? 

2 thoughts on - JE! NI KWELI KUWA KRISTO ALIFUFUKA SIKU YA PASAKA KULINGANA NA MAANDIKO?

LEAVE A COMMENT