SWALI: Je! Ni kweli kuwa, maandiko matakatifu ni jumla ya vitabu 66?
JIBU: Jibu ni hapana, si Kweli kwamba, maandiko Matakatifu ni jumla ya vitabu 66 tu, la hasha! Bali ni zaidi ya hivyo, ukiachilia tu mbali vile ambavyo havijaandikwa kuhusu yale yaliyofanywa na Bwana ambapo ulimwengu nzima usingetosha kwa wingi wa vitabu (Yohana 21:25),
Lakini kwa yale tu yaliyoandikwa yenyewe ni zaidi ya hivyo 66, na baadhi vilitumika na kutumiwa na watumishi wa Kristo wa wakati huo mfano Yuda nduguye Yakobo, ambaye alinakili sehemu ya maandiko matakatifu yasiyopatikana katika kitabu cho chote kile kati ya vile 66 (soma Yuda 1:14), au vitabu vile vilivyoandikwa na manabii watakatifu kama vile kitabu cha maelezo cha nabii Ido, kitabu cha cha nabii Samweli, kitabu cha nabii Gadi, kitabu cha nabii Nathani, waraka wa Yeremia n.k, ambavyo tunavisoma katika
2 Mambo ya Nyakati 13:22 Na mambo ya Abiya yaliyosalia, na njia zake, na maneno yake, yameandikwa katika KITABU CHA MAELEZO CHA NABII IDO.
Na
1 Mambo ya Nyakati 29:29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo na mwisho, angalia, zimeandikwa katika TAREHE YA SAMWELI, MWONAJI, na katika TAREHE YA NATHANI, NABII, na katika TAREHE YA GADI, MWONAJI;
Na
Yeremia 29:1 Maneno haya ndiyo maneno YA WARAKA, ambao NABII YEREMIA aliupeleka toka Yerusalemu, kwa hao waliobaki wa wakuu waliochukuliwa mateka, na kwa makuhani, na kwa manabii, na kwa watu wote, ambao Nebukadreza aliwachukua mateka toka Yerusalemu hata Babeli;
Na hayo yote ni maandiko matakatifu na yenye pumzi ya Mungu, na yalitumika na watu wa Mungu wa Wakati huo (wakiwemo mitume na Bwana Mwenyewe), na tena manabii hao watakatifu hawakuandika vitabu hivyo kwa mapenzi yao, bali waliongozwa na Roho aliyekuwa ndani yao, na zaidi sana sana Bwana Yesu alisema tuyaamini YOTE yaliyosemwa na manabii hao.
Luka 24:25 Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini YOTE WALIYOYASEMA MANABII!
26 Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?
Na katika kuwaeleza wale watu wawili waliokuwa wakielekea Emau mambo yaliyo muhusu Yeye, alirejea maandiko ya Musa na ya MANABII WOTE.
27 Akaanza kutoka Musa na MANABII WOTE, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe.
(Hapo anasema maandiko ya MANABII WOTE na sio maandiko ya manabii fulani tu)
Na si hivyo tu, hata kwa wakristo waliokuwepo wakati wa mitume, walikuwa na maandiko, au vitabu, au nyaraka zaidi ya zile zilizopo kwenye vitabu 66 (soma Wakolosai 4:16 utathibisha hilo).
Wakolosai 4:16 WARAKA HUU ukiisha kusomwa kwenu fanyeni kwamba usomwe katika kanisa la Walaodikia pia; NA ULE WA LAODIKIA USOMWE NA NINYI.
Hivyo, maandiko matakatifu yaliyoandikwa ni zaidi ya vitabu 66, na YOTE hayo yaliyotangulia kuandikwa yaliyandikwa ili kutufundisha sisi.
Warumi 15:4 KWA KUWA YOTE YALIYOTANGULIA KUANDIKWA YALIANDIKWA ILI KUTUFUNDISHA SISI; ILI KWA SABURI NA FARAJA YA MAANDIKO TUPATE KUWA NA TUMAINI.
Na yale yote yalifunuliwa yalifunuliwa kwa kwa ajili yetu sisi ili tupate kuitii sheria ya Kristo kama ilivyoandikwa katika
Kumbukumbu La Torati 29:29 Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; LAKINI MAMBO YALIYOFUNULIWA NI YETU SISI NA WATOTO WETU MILELE, ILI TUFANYE MANENO YOTE YA SHERIA HII.
Hapo Anaposema ili tuyafanye maneno ya SHERIA HII maana yake ni sheria ya Kristo (Wagalatia 6:2), kwa sababu manabii walinena habari za Kristo, na Musa naye alisema tumsikilize Yeye atakayekuja yaani Kristo (Matendo 3:22).
Hivyo kuwa na bidii na tabia ya kusoma na kujifunza biblia yako kwa kumwomba Mungu kukusaidia kuitii injili kwani huko ndiko kwenye wokovu wa roho yako.
Bwana akubariki, Shalom.
Mada zinginezo:
FUNZO KUTOKA KATIKA KISA CHA NADABU NA ABIHU.
INJILI YA KRISTO HAIENDI NA WAKATI
UMEMWAMINI YESU KRISTO KWA NAMNA GANI?
JE! NI DHAMBI KWA MWANAMKE NA MWANAMUME KUISHI PAMOJA PASIPO KUFUNGA NDOA KIBIBLIA?

5 thoughts on - JE! NI KWELI KUWA MAANDIKO MATAKATIFU NI JUMLA YA VITABU 66?
mtumishi, nimefanya dhambi ya uzinzi kwa makusudi kabisa yaani mwanzo nilikuwa nikiwaza kuhusu ngono kwakuwa nilikuwa sijaifanya mwanzo mpaka imenipelekea kusikia sauti ndani yangu ikiniambia mtakufa bila kularaha ya dunia mpaka ikanipelekea kuzini nakwafursa hiyo kufanya dhambi nyingine mingi kwa makusudi sasa hivi nikitaka kutubu nitasamehewa kweli? maana naisi kufa hivi na upweke ndani yangu
Ukitubu utasamehewa kabisa mpendwa, je! Ulishamwamini Kristo kabla na kubatizwa kwa jina lake?
Ndio nimekwisha kumwamini na kwanza niliokoka mwezi wanane mwaka uliopita, na nina miaka 18, na katika familia yetu mimi pekee ndiye mkristo na tangu wakati huho nilikuwa nikisoma biblia nakumaliza agano jipya yote nakujifunza mafundisho yote ya wingulamashahidi.org lakini katika sikuhizi nimeshangaa kuona tabia nyingi mbaya zikihinuka ndani yangu hadi kufikia kufanya uzinzi nahivi nilitoka kutafuta mchungaji sikumuona nahivo naomba munisaidie kwamaombi pia kwakuwa naisi kufa hivi sina amani hatakidogo naisi kufa.
Unachopaswa kufanya ni kwenda mbele za Mungu Kuomba toba, au wasiliana nasi kwa namba za simu
pale mtu anapofanya dhambi anawezafanyanini ili awezetena kuokoka?