Hii ni maana ya kuota umepotea mahali

Ndoto No Comments

Nakusalimu katika Jina la Yesu Kristo, Bwana wetu.

Unapoota umepotea iwe ni njia panda, mjini, shambani, katika riadha ama sehemu yoyote Ile usiyoijua, basi tambua hizo ni ndoto zilizobeba ujumbe kutoka kwa Mungu kwa makundi yote yaani walio okoka na hata wale wasio okoka.

Biblia inasemaje kuhusu ndoto hii kwa ambae Hajaokoka

Zaburi 37:18-20

18 ”Bwana anazijua siku za wakamilifu, Na urithi wao utakuwa wa milele.

19 Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba.

20 Bali wasio haki WATAPOTEA, Nao wamchukiao Bwana watatoweka, Kama uzuri wa mashamba, Kama moshi watatoweka.”

Unaona, njia ya wasio HAKI siku zote ni kupotea, hivyo kuota umepotea ni Ujumbe kutoka kwa Mungu wako kuonesha Hali yako kiroho kwamba umepotea. Jinsi unavoona katika ndoto unahangaika huku na kule, Unaoneshwa itakavyokuwa mateso ya kulitafuta neno na usilipate, mpendwa ni nyakati mbaya sana hizo na itakuwa tayari umeshachelewa kumgeukia Bwana kipindi hiko

Zaburi 1:6

” Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.”

Mungu anakupenda, Naam, ndiposa anakuonesha mambo haya ubadilike njia zako mapema Leo hii, Leo upo hai lakini kesho huenda ikawa si yako mpendwa. Huenda upo mahali pazuri una familia nzuri, kazi nzuri, nyumba, Afya nzuri n.k lakini hakika Umepotea! Unachopaswa kufanya ni kumgeukia Mungu wako ili Akuokoe, nae atakuonesha njia Ambayo ni kweli na Uzima yaani Yesu Kristo.

Yohana 14:6

” Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”

Na hivyo Amekuja kuokoa kilichoptea {Mimi na wewe}

Mathayo 18:10-11

10 ”Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.

11 [Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.]”

Ikiwa Leo utakuwa tayari kumkabidhi Kristo maisha yako, basi yeye ni mwaminifu atakuokoa na kukusamehe. Hapo ulipo chukua muda mfupi tafakari Maovu kiasi Gani umemfanyia Mungu wako? Kwa Imani zungumza na Mungu Mwombe rehema, usifiche uovu wako, maanisha kumuomba yeye akusamehe maana yu karibu Anasikia. Kwa Toba itokayo moyoni kwa dhati kabisa kwamba upo tayari kuacha maisha yako ya dhambi, Basi fahamu kwa hivyo tu Mungu amekusamehe.

Baada ya hapo tafuta ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo ( Matendo 2:38) upate ondoleo la dhambi na utimize HAKI yote kama mwana wa MUNGU. Kwa hayo Mungu atakumwagia kipawa Cha Roho mtakatifu.

Maana kwa Aliyeokoka

Ikiwa umeshaokoka au mwamini na unakutana na ndoto za Namna hii basi Mungu anakukumbusha kuwa utaiacha njia yako ya wokovu, aidha kwa uamuzi utakaoufanya hivi karibuni au umeshaanza kufanya au Huenda kuna dhambi unayoitenda sasaivi Ambayo ni machukizo mbele za Mungu. Kuwa makini sana na kuishika taji uliyonayo shetani asije itwaa thawabu yako

Ezekieli 44:9-10

9 ”Bwana MUNGU asema hivi; Hapana mgeni, ambaye moyo wake haukutahiriwa, wala mwili wake haukutahiriwa, atakayeingia patakatifu pangu, miongoni mwa wageni walio kati ya wana wa Israeli.

10 Lakini Walawi waliofarakana nami, hapo Waisraeli walipopotea, waliopotea na kuvifuata vinyago vyao, watachukua uovu wao wenyewe.”

Hivyo usirudi nyuma Tena mpendwa na ukumbuke Bwana alipokutoa. Maana Mungu anakupenda ndio Maana anakuonya hivyo mtii kwa kuyaacha maisha ya dhambi uliyoyaishi kabla. Tutafute kwanza uwepo wa Mungu ndani yetu hayo mengine ya Dunia hii hayana umuhimu kuliko Yale ya kristo Yesu.

Maranatha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *