Kuhusu sisi

Rejeabiblia.com ina chimbuko kutoka wingulamashahidi.org.

Tovuti hii imeanzishwa mahususi kwa ajili ya kutoa mafunzo ya biblia kwa kina katika lugha rahisi inayoweza kueleweka kwa makundi yote ya watu.

Utakutana na maswali mengi ya biblia yaliyojibiwa, ikiwemo kupewa wigo wa kuuliza maswali yako katika box letu la maoni chini.

Rejeabiblia.com haifungamani na dhehebu lolote, Bali inajitegemea ikiwa na lengo la kuyafikisha maarifa ya biblia kwa watu wote bure.

Tunaamini Biblia ndio kitabu pekee kilichovuviwa na Roho Mtakatifu, chenye hatma yote ya maisha ya mwanadamu kuanzia akiwa hapa duniani hadi kule ng’ambo atakapofika.

Tunaamini wokovu unapatikana kwa mmoja tu naye ndiye YESU KRISTO BWANA wetu na kwamba ili mtu aokoke ni sharti amwamini, na kubatizwa na kupokea Roho Mtakatifu. Sawasawa na (Yohana 14:6, Matendo 2:38)

Tunaamini Mungu ni mmoja tu, aliyejifunua na kutenda kazi katika ngazi kuu tatu yaani (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu). Kumbukumbu 6:4, 1Yohana 5:8

Tunaamini katika unyakuo wa kanisa na kurudi kwa pili kwa Kristo duniani. Na kwamba wakati tuliopo ni wa siku za mwisho. Hivyo ni wajibu wa kila mwanadamu kujiweka tayari kwa ajili ya kumlaki Bwana Yesu mawinguni.

Mwisho Rejea.com inafungua wigo kwa kila mtu anayeguswa kuchangia maarifa haya kwa njia ya kiuandishi au ya kifedha ili kufanikisha utunzaji huu wa maarifa kwa vizazi vijavvyo vya mbeleni.

Twashukuru kwa kuitembelea tovuti hii.

Bwana akubariki na uwe na usomaji mwema.