Archives : May-2024

Hapa Biblia inatuonyesha bidii inamkweza/mpandisha mtu, bidii inayozungumziwa hapa kwenye maandiko imeenda mbali zaidi ya ile bidii ya kufanya kazi kwa kipindi kirefu, lakini ni ile bidii ya kutoa na kutumia ujuzi na ufanisi kwa jambo ulilopewa kulitenda kwa muda, wenye utashi kama huo mara nyingi wanachukua usikivu na kuwateka macho wenye vyeo na wafalme ..

Read more

Msemo huu umekuwa ukionekana umeekwa kwenye sehemu mbalimbali ya vifungu vingi vya maandiko, Tuangalie hapa, Kutoka 23:18-19[18]Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi. [19]Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika ..

Read more

Maana halisi ya neno kuwiwa ni “kudaiwa”. Kwa mfano ukisikia Mtu anasema anawiwa kiasi fulani cha fedha maana yake ni kwamba mtu huyo anadaiwa kiasi fulani cha fedha au anawiwa na mtu mwingine kiasi fulani cha fedha vivyo hivyo anamaanisha anamdai mtu fulani kiasi fulani cha fedha.. Hivyo kwa kiswahili fasaha neno kuwiwa/ kuwia ni ..

Read more

JIBU: Vyano ni wingi wa neno chano maana yake ni sinia. Katika andiko hilo tunaona mwandishi anasema neno linenwalo wakati wa kufaa ni kama machungwa katika vyano vya fedha akimaanisha ni kama machungwa katika masinia ya fedha. Utajiuluza iweje mwandishi afananishe neno linalofaa na machungwa katika masinia ya fedha? Kuna aina ya machungwa yanayopatikana katika ..

Read more

Jaa ni eneo maalum ambalo limetengwa kwa ajili ya kuhifadhi takataka , taka hizo zinaweza kuwa zitokanazo na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama taka za viwandani, mahospitali, pamoja na majumbani. Maeneo yote hayo uchafu (taka) unaweza kupatikana kutokana na shughuli za mbalimbali zinazofanyika. Pia uchafu waweza kuwa unaotokana na vinyesi vya wanyama ( yaani mbolea) ..

Read more

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu karibu tuyatafakari maneno ya uzima. Kama mwamini uliyemuamini Yesu Kristo kweli kweli na kusimama thabiti katika imani kwa muda mrefu na Kristo ziko dalili ambazo ukiziona hizo ndani yako jua kabisa kama usipokuwa makini na kutaka kupiga hatua mbele jua kabisa unakwenda kuanguka tena anguko kubwa sana. Tutakwenda ..

Read more

Neno Sharoni maana yake ni “uwanda” au “nchi tambarare”. Katika maandiko tunaona kuna eneo(wilaya) ambalo linajulikana na kufahamika sana na waisraeli kama sharoni ijapokuwa katika biblia hakuna maelezo mengi yaliyotolea kuhusu eneo hilo. Ingawa ni eneo ambalo lilikuwa na rutuba nyingi, na pia lipo karibu sana na fukwe za bahari kubwa ya Mediterenia , waweza ..

Read more

Maana ya Neno mintarafu,lina maanisha “Kuhusiana na”  mfano mzuri ukitaka kutamka sentesi inayosema, Sielewi chochote kuhusiana na kurudi kwa Yesu Kristo, unaweza kusema” Sielewi chochote mintarafu  kurudi kwa Yesu Kristo, hivyo kiwakilishi cha Mintarafu ni sawa na Neno, Kuhusiana na, Ndani ya biblia takatifu yenye vitabu 66, Neno hili limeonekana mara mbili, kwenye kitabu cha ..

Read more

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo. Watu wajikatao wanaozungumziwa hapa ni Wayahudi yaani wafanyao TOHARA. Ambacho ni kitendo cha kukata sehemu ya mbele ya viungo vya uzazi vya mwanaume. Sasa hawa wajikatao yaani Wayahudi walikuwa wakiwataabisha watu na kuwashurutisha watu ambao sio Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo. Wakiwataka wafanyiwe tohara kama jinsi torati ilivyoagiza ..

Read more