Maana Ya neno JAA nini katika biblia ?

Maswali ya Biblia No Comments

Jaa ni eneo maalum ambalo limetengwa kwa ajili ya kuhifadhi takataka , taka hizo zinaweza kuwa zitokanazo na shughuli mbalimbali za kibinadamu kama taka za viwandani, mahospitali, pamoja na majumbani.

Maeneo yote hayo uchafu (taka) unaweza kupatikana kutokana na shughuli za mbalimbali zinazofanyika. Pia uchafu waweza kuwa unaotokana na vinyesi vya wanyama ( yaani mbolea) wafugwao ambao pia waweza lundikwa, kwa muda wa kipindi fulani. Hivyo kwa ufupi maeneo yanayotengwa Kwa ajili ya kutupa taka yanajulikana kama madampo au majalala utofauti wa majina ni kutokana na kiwango cha taka kilichopo katika eneo husika. Kwa hiyo neno JAA kwa maana nyingine ni kama jalala tu..

Tukisoma katika biblia tunaona neno hili likitumika. Katika kitabu cha:

Tukisoma katika biblia tunaona neno hili likitumika. Katika kitabu cha:

Zaburi 133: 7 “Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani”.

Maana yake Bwana anaweza kumtoa mtu kutoka majalalani na kumpandisha juu.

Ezra 6: 11 “Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili”.

Isaya 25: 10 “Kwa maana mkono wa Bwana utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika MAJI YA JAA”

Pia unaweza kusoma Danieli 2:5, Danieli 3:39, Maombolezo 4:5 na 1Samweli 2:8.

Katika Agano jipya neno hili limetumika mara moja tu, na Bwana Yesu Kristo katika kitabu cha Luka..

Tusome..

Luka 14:34 “Chumvi ni kitu chema; lakini chumvi ikiwa imeharibika, itiwe nini ikolee?

35 Haiifai nchi WALA JAA; watu huitupa nje Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie”

Hata hivyo Kinyesi cha wanyama kinapozidi kukaa sana na kuharibika kinafaa kwa matumizi ya mbolea, watu wanakikusanya na kukitumia kama mbolea kwa baadaye, hali kadhalika baadhi ya takataka nyingine zinavyozidi kuharibika huwa hazikosi matumizi, nyingine zinaweza hata kutumika katika kuzalisha gesi ya asili, ambayo itatumika kama nishati mbadalaa.

Walakini kwa chumvi ni kitu cha ajabu na cha utofauti maana pale ambapo chumvi uharibika kamwe haiwezi tumika tena kwa matumizi ya aina yeyote kwenye chakula , haina mbadala wa matumizi kama vile takataka nyingine kama kinyesi cha wanyama na baadhi ya taka kama makopo ya plastiki yanaweza okotwa tena na kutumika tena .Kwaufupi inakuwa kama mchanga tu..

Kwa hiyo Bwana Yesu alitufananisha sisi, tuliompokea yeye na chumvi..

Mathayo 5:13 “Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.

14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima”.

Pia sisi tulimpokea Yesu Bwana anatuonya, tujihadhari tunavyoenenda katika ulimwengu huu matendo yetu yasije yakatuharibia sifa zetu moja kwa moja, hata tusifae tena mbele za Mungu na wanadamu.

Bwana akubariki.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *