Fahamu maana ya Mithali 25: 11 “Neno linenwalo wakati wa kufaa, Ni kama machungwa katika vyano vya fedha”.

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU:

Vyano ni wingi wa neno chano maana yake ni sinia. Katika andiko hilo tunaona mwandishi anasema neno linenwalo wakati wa kufaa ni kama machungwa katika vyano vya fedha akimaanisha ni kama machungwa katika masinia ya fedha. Utajiuluza iweje mwandishi afananishe neno linalofaa na machungwa katika masinia ya fedha?

Kuna aina ya machungwa yanayopatikana katika nchi za mashariki ambayo ni matamu sana kuliko nchi zote duniani, juisi yake ni tamu na ina harufu nzuri sana. Machungwa hayo hayawezi kusafirishwa nje ya nchi kwa sababu hayawezi kukaa kwa mda mrefu bila kuharibika,na kwa tamaduni za huko huyavuna na kuyaweka katika masinia. Machungwa haya yalikuwa maalumu kwa ajili ya watu walio na uchovu mwingi , na wakati wa chakula juisi yake iliwaburudisha na kutoa uchovu wao. Ni mfano wa kipindi hichi upewe soda iliyo Katika ubaridi wakati wa jua kali itakubudurisha,hakika,Basi ilikuwa hivyo kwa watu wanaoshi nchi za mashariki ya kati na katika baadhi ya maeneo ya Asia…

Hivyo basi neno zuri linaloweza kumfariji mtu wakati wa uchungu au msiba, au neno lenye kutia moyo lilivyo na thamani kwa mtu aliyevunjika moyo ni kama machungwa kwenye masinia ya fedha kwa ajili ya waliochoka.Maneno haya mazuri ya kufariji, kujenga kuimarisha, kuponya hayatoki kwingine isipokuwa kwa mmoja tu Yesu Kristo pekee.

Tunapowahubiria wengine habari za Yesu zinawaponya kuliko habari nyingne zozote walizowahi kuzisikia kwa sababu Yesu mwenyewe alikuja kwa ajili hiyo.

Isaya 61:1-3
[1]Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.


[2]Kutangaza mwaka wa BWANA uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;


[3]kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.

Hivyo basi, tuwahubiri watu habari njema za Yesu Kristo ili wapate uponyaji. Ukiwa mtu wa kuwasaidia wengine kumjua Kristo utatuzi wa mambo yote ataupata maana ndani ya Yesu tunapata wokovu na zaidi sana tunapata furaha na amani ya kweli idumuyo, tukifanya hivyo Mungu anatuona kama watu wenye kutoa huduma ya machungwa yaliyo katika masinia ya vyombo fedha…

Bwana Yesu atusaidie kwa Neema yake tuweze kuyatendea kazi yote…

Shalom…

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *