Fahamu maana ya neno “KUWIWA”

Maswali ya Biblia No Comments

Maana halisi ya neno kuwiwa ni “kudaiwa”. Kwa mfano ukisikia Mtu anasema anawiwa kiasi fulani cha fedha maana yake ni kwamba mtu huyo anadaiwa kiasi fulani cha fedha au anawiwa na mtu mwingine kiasi fulani cha fedha vivyo hivyo anamaanisha anamdai mtu fulani kiasi fulani cha fedha.. Hivyo kwa kiswahili fasaha neno kuwiwa/ kuwia ni kudaiwa au kudai kitu au jambo fulani.

Tukisoma Katika maandiko tunaona mifano kadhaa ambayo neno hili limetumika:

Mathayo 18: 22 “Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.

23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.

24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.

25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyo navyo, ikalipwe ile deni

26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.

27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni”.

Mistari mingine katika biblia yenye neno hilo “kuwiwa” ndani yake ni Luka 16:7 na Warumi 13:8.

Hata na sisi pia maandiko yanatufundisha kuwa tukishakuwa tumefanyika viumbe vipya yaani baada ya kuokoa sisi pia tunadeni na ni wajibu wetu moja kwa moja kwenda kuwatangazia wengine habari njema za Bwana wetu Yesu kristo. Hivyo TUNAWIWA na sisi kwa watu wa ulimwenguni kwenda kuwa tangazia injili.

Hivyo niwajibu wetu kuipeleka injili kwa watu wengine, ambao bado hawaja fahamu kweli kwa kupitia karama , mali na kwa nguvu zetu, kwasababu hilo ni deni kwetu.

Kamavile ambavyo Mtume Paulo alivyosema katika maandiko ya kwamba ANAWIWA na watu wa aina mbali mbali, katika kuwapelekea injili..

Hata na sisi pia maandiko yanatufundisha kuwa tukishakuwa tumefanyika viumbe vipya yaani baada ya kuokoka sisi pia tunadeni na ni wajibu wetu moja kwa moja kwenda kuwatangazia wengine habari njema za Bwana wetu Yesu kristo.

Hivyo TUNAWIWA na sisi kwa watu wa ulimwenguni kwenda kuwa tangazia injili. Hivyo niwajibu wetu kuipeleka injili kwa watu wengine, ambao bado hawaja fahamu kweli kwa kupitia karama, mali na kwa nguvu zetu, kwasababu hilo ni deni kwetu, kama vile ambavyo Mtume Paulo alivyosema katika maandiko ya kwamba ANAWIWA na watu wa aina mbali mbali, katika kuwapelekea injili..

Warumi 1:13 “Lakini, ndugu zangu, sipendi msiwe na habari, ya kuwa mara nyingi nalikusudia kuja kwenu, nikazuiliwa hata sasa, ili nipate kuwa na matunda kwenu ninyi pia kama nilivyo nayo katika Mataifa wengine.

14 NAWİWA NA WAYUNANİ na wasio Wayunani, NAWİWA na wenye hekima na wasio na hekima.

15 Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi ni tayari kuihubiri Injili hata na kwenu ninyi mnaokaa Rumi.

16 Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia”.

Hivyo Kuhubiri injili kwa watu wengine ambao hawajaokoka ni moja ya wajibu wetu kwa sisi ambao tayari tumekwisha mpokea Bwana Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha Yetu. Kwa Maana tunafanyika kuwa watenda kazi katika shamba la Bwana kusudi kuweza kuokoa roho za watu zilizopotea .

Hivyo ni lazima kuwapelekea habari njema za wokovu pasipo kuionea haya injili, kwasababu injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu, na tunalidhibitisha Hilo katika maandiko kwenye kitabu cha:

Marko 16: 15 “Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa”.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *