Elewa maana ya “Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake,

Maswali ya Biblia No Comments

Msemo huu umekuwa ukionekana umeekwa kwenye sehemu mbalimbali ya vifungu vingi vya maandiko,

Tuangalie hapa,

Kutoka 23:18-19[18]Usisongeze damu ya dhabihu zangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala mafuta ya sikukuu yangu usiyaache kusalia hata asubuhi.

[19]Ya kwanza ya malimbuko ya nchi yako utayaleta na kuyatia ndani ya nyumba ya BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake..

Tukisoma tena

Kutoka 34:25-26[25]Usisongeze damu ya sadaka yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu; wala hiyo sadaka ya sikukuu ya pasaka haitasazwa hata asubuhi.

[26]Vitu vya kwanza vya malimbuko ya nchi yako utavileta na kuvitia ndani ya nyumba ya BWANA Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake

.

Tunaona tena kwenye

Kumbukumbu la Torati 14:21[21]Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.

Maandiko yanaposema usimtokose mwanambuzi Katika maziwa ya mama yake, anamaanisha  kumchemsha mwana mbuzi kwa maziwa ya mama yake,badala ya kutumia maji Katika kumchemsha,unayatumia maziwa ya mama yake anayoyanyonya na kumchemshia…

Kiuhalisia sio kitendo kizuri au chenye kuleta picha nzuri, utajiuliza kwanini ufanye hivyo? Ni kwamba hakuna maji ya kumchemshia au namna nyingine hata kuyatumia maziwa ya mama yake, ni sawa na nguruwe aliyezaa Watoto wake baada ya hapo uanze kuwapa awale watoto wake, ndilo hilo linalozungumziwa hapo..

Ni kitendo kibaya na kinachoonyesha kukosa nidhamu hata kwa viumbe vya Mungu..

Utaratibu huu ulikuwa unafanywa na wapagani, watu wasio mjua Mungu, na waliyafanya yote haya kwasababu ya imani zao kishirikina, ni kama mila na matambiko yanayoendelea kwa kipindi cha sasa, ndo mana Mungu aliwaonya wana wa Israel wasifanye haya kwasababu ni machukizo mbele zake, desturi hii haina tofaina ule utaratibu wa kuwapitisha Watoto kwenye moto (soma 2Wafalme 21:6, 2Wafalme 16:3).

Kwa nyakati hizi pia, Kafara kama hizi zinafanyika rohoni,

Tunapofanya mambo yasiyo mpendeza Mungu huku tukimtolea dhabihu, tufahamu tunafanya mambo kama watu Mataifa, tunapomtolea Mungu sadaka zetu na huku tunafanya biashara zilizo haramu, tunasema tunaenda kanisani lakini tuna ushirikina ndani yetu,ni wachawi, hivyo pia tunaposema tumeokoka na huku hatuwaheshimu wazazi wala wakubwa kwa wadogo,tunasema tunamwimbia Mungu kwa vinywa vyetu ila midomo Yetu imejaa matusi, uwongo, usengenyenyaji,na visasi tufahamu kabisa,(hiyo yote katika roho ni sawa na kumtokosa mwanambuzi katika maziwa yake)

Ni mapenzi ya Bwana tuzidi kushika amri zake na sheria zake ili tuzidi kumpendeza zaidi,

Bwana Yesu atuokoe..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *