Fahamu maana ya Mithali 22:29 “Je! Wamwona mtu mwenye bidii katika kazi zake? Huyo atasimama mbele ya wafalme,

  Maswali ya Biblia

Hapa Biblia inatuonyesha bidii inamkweza/mpandisha mtu, bidii inayozungumziwa hapa kwenye maandiko imeenda mbali zaidi ya ile bidii ya kufanya kazi kwa kipindi kirefu, lakini ni ile bidii ya kutoa na kutumia ujuzi na ufanisi kwa jambo ulilopewa kulitenda kwa muda, wenye utashi kama huo mara nyingi wanachukua usikivu na kuwateka macho wenye vyeo na wafalme kwa utendaji wao..

Tuchukulie mfano ni wafanyakazi wa shirika fulani,wanatenda kazi kwa ufanisi wa juu, na kutimiza utendaji wa kazi kwa muda waliowekewa, sasa watu kama hawa huwa wanapendwa na maboss zao na kupewa vipaumbele kwa kuongezewa cheo hata na mshahara pia..Pia watu ambao ni wagunduzi Katika kuleta mabadiliko kwenye jamii wanapewa fursa za kualikwa na viongozi, pamoja na maraisi kwa kupewa pongezi hata wakati mwingine wanafanywa kuwa washauri wa Mambo yanayoendelea au kujitokeza..

Andiko hili linafunua nini kiroho?

Na sisi ili tupate kibali cha kukubalika mbele Mungu wa Miungu, Mfalme wa wafalme,ambaye ni zaidi ya wakuu wote na wafalme wote wa duniani, ambaye ni YESU KRISTO, hivyo hatuna budi Kumpenda yeye na Kumtumikia kwa kuyafanya mapenzi yake, haleluya..

Bwana Yesu anasema..

Kumbukumbu 28:1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, KWA BIDII, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani

Tukiwa hatuna ulegevu,ni ahadi ya Bwana kutunyanyua juu zaidi, ahadi yake haiwezi kutanguka,tukionyesha bidii kwake..

Warumi 12:11  ‘kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;’

Jihakikishie unatumia Akili yako,nguvu zako,roho yako na moyo wako Katika kumtumikia Mungu,hakikisha unatumia vyote kwa muda mchache ambao umepewa duniani,angalia unakitendea kazi na Kwa namna gani utakiweka kitaleta matokea mema mbele za Bwana,fanya vyote kwa kutumia ujuzi,bidii na maarifa…

Ikiwa upo nje ya Yesu Kristo, fahamu kabisa huwezi kumtumikia Mungu, lazima uokoke kwanza…

Bwana akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT