Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ni ipi?

Uasherati ni kitendo cha kufanya zinaa nje ya ‘kifungo cha ndoa’. Hii ikilenga makundi yote ya watu, yaani kwa mtu ambaye hajaoa/hajaolewa na kufanya kitendo hicho.. Na kwa mtu ambaye tayari ameshaoa/ ameshaolewa, lakini akaenda kufanya kitendo hicho na mtu mwingine ambaye hakufunga naye ndoa. Vyote hivyo ni vitendo vya uasherati.. kwasababu vyote vipo nje ya ndoa.

Tofauti na Neno uzinzi, ambalo lenyewe limeegemea kwa wanandoa tu. Yaani Mwanandoa kutoka nje ya ndoa yake. Huyo anafanya aina ya uasherati inayoitwa “Uzinzi”

Lakini  Neno uasherati bado haliishii tu kwenye kufanya zinaa kama inavyozoeleka, bali linakwenda mbali zaidi kujumuisha vitendo vya kuingiliana kinyume na maumbile, kulala na wanyama, kufanya punyeto, kutumia vifaa vya ngono(midoli) kama mbadala wa mwanadamu n.k..vyote hivyo vinajumuishwa katika uasherati.

 Hivyo sehemu nyingine, biblia inaweza tumia Neno uasherati, lakini limelenga uzinzi kwa wanandoa.. Sehemu nyingine inakwenda moja kwa moja, inategemea na habari husika iliyokuwa inalengwa..

Lakini pamoja na hayo biblia inasema waasherati na wazinzi wote mwisho wao ni hukumu ya moto milele.

Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu”.

Ufunuo 21:8 “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Je! Na wewe bado upo katika maisha ya namna hii? Kama ndio, kumbuka ukifa leo, huna namna ambayo utakwenda ziwa la moto. Hivyo ni heri umkaribishe Bwana Yesu maishani mwako leo, kwa nguvu zako mwenyewe hutaweza. Lakini Bwana Yesu anaweza kukusaidia kuyashinda hayo yote.Endapo tu utamaanisha kabisa kwa dhati kutoka katika moyo wako, kumkaribisha maishani mwako, Yeye mwenyewe atakupa nguvu ya kuweza kuyashinda hayo yote, kwa neema yake. (Yohana 1:12)

Hivyo kama upo tayari kwa ajili ya kuongozwa sala ya Toba. Unaweza kubofya hapa, kwa ajili ya mwongozo.>>

Bwana akabariki.

6 thoughts on - Tofauti kati ya uzinzi na uasherati ni ipi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *