Hao wajikatao ni akina na nani? Wafilipi 3:1.

Maswali ya Biblia No Comments

Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Watu wajikatao wanaozungumziwa hapa ni Wayahudi yaani wafanyao TOHARA. Ambacho ni kitendo cha kukata sehemu ya mbele ya viungo vya uzazi vya mwanaume.

Sasa hawa wajikatao yaani Wayahudi walikuwa wakiwataabisha watu na kuwashurutisha watu ambao sio Wayahudi waliomwamini Yesu Kristo. Wakiwataka wafanyiwe tohara kama jinsi torati ilivyoagiza kwamba wakitahiriwa yaani tohara ya mwilini itawafanya wakubaliwe na Mungu.

Sasa ukisoma kwenye biblia ya kiingereza(Amplified Bible) imeeleza vyema hebu tusome.

Philippians 3:2
[2]Look out for those dogs [Judaizers, legalists], look out for those mischief-makers, look out for those who mutilate the flesh.

“Judaizers legalists” maana yake ni Wayahudi wanasheria au washika sheria yaani torati.

Ukisoma pia hapo utaona neno “mutilate flesh” maana yake wakatao/wakata viungo.

Wafilipi 3:1 ‘Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi.

2 Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na WAJIKATAO’’.

3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili’.

Jambo ambalo si kweli ukija katika agano bora ambalo ni agano jipya. Na tohara ya agano hili jipya ni tohara ya rohoni ndio iliyokubalika na Mungu na sio ya mwilini kama ilivyokuwa kipindi cha kina Musa.
Na tohara yenyewe ni “Ubatizo wa Roho Mtakatifu ” ambae ndie Yesu Kristo anakuja kukaa ndani yetu na kututoka katika sheria ya mauti ambayo ndio tohara na kutupeleka katika katika sheria ya Roho wa uzima!.

Sasa Roho Mtakatifu anapokuja kukaa ndani yetu anaondoa ile sehemu ya nyama iliyozidi katika mioyo yetu ambayo ni kiburi,tamaa mbaya,wizi,uasherati,uzinzi,chuki,husuda nk.
Anaondoa kila aina ya dhambi na kutufanya wakamilifu.

Hivyo mtu anaefanyiwa tohara katika agano jipya huyo ni wa Mungu kama maandiko yanavyosema.

Warumi 8:9 ‘Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, HUYO SI WAKE’.

Unaona hapo anasema!, “…..lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo huyo si wake”

Kama tu katika agano la Kale ambae alikuwa hajatahiriwa huyo alikuwa si wa Mungu na waliokuwa wametahiriwa basi huyo ni wa Mungu.

Hivyo Mtume Paulo alikuwa akiwaonya watu waliokuwa sio Wayahudi waliomuamini Yesu Kristo kwamba kutahiriwa mwilini sio kigezo cha kukubaliwa na Mungu kama wajikatao walivyokuwa wakiwadanganya na kuwashurutisha.

Wagalatia 6:15 ‘Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya’.

Hiyo ikimaanisha kuwa sisi ni kitu kimoja katika Kristo Yesu sio myahudi,muafrika,mchina tukiisha mwamini Yesu Kristo hatuhitaji tohara ya mwilini ili tukubalike na Mungu maana hatuko katika agano jipya.

Hivyo kumwamini Yesu Kristo na kupokea Roho Mtakatifu na kutembea nae katika ukamilifu wote na kubatizwa katika ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo ndio kuzaliwa mara ya pili yaani tohara ya rohoni.

Je! Umezaliwa mara ya pili?
Kama bado unasubili nini? Fanya uchaguzi ulio bora na wa milele.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >>

https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *