Tafsiri ya Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake;

Maswali ya Biblia No Comments

Mithali 12:10 “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake; Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili”.

Mahali hapa Mungu alitutaka tujue sifa za mtu mwenye haki, au tabia ya mtu mwenye haki mara nyingi huwa na huruma kwa Kila kitu, na huwa haishii kuonyesha huruma kwa wanadamu tu bali hata kwa wanyama pia

Na ndiyo tabia ambayo Mungu anayo siku zote hukakikisha kuwa wanyama wote wanakuwa salama, na hukikisha hakuna hata mnyama mmoja anakufa pasipo yeye kujua, jambo hili unaweza kusoma hapa

Mathayo 10:29 “Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;”

Hata katika habari ya baalamu, wakati alikuwa njiani akiwa pamoja na punda wake tunaona pale punda alipogoma kwenda alimpiga mara tatu, lakini tuona baada ya malaika kufika pale alimuuliza Balaamu kwanini anampiga punda namna hiyo

Hesabu 22:26-32

[26]Malaika wa BWANA akaendelea mbele akasimama mahali pembamba sana, hapakuwa na nafasi ya kugeukia mkono wa kuume, wala mkono wa kushoto.

[27]Yule punda akamwona malaika wa BWANA, akajilaza chini ya Balaamu; hasira yake Balaamu ikawaka, akampiga punda kwa fimbo yake.

[28]BWANA akakifunua kinywa cha yule punda, naye akamwambia Balaamu, Nimekutenda nini, hata ukanipiga mara tatu hizi?

[29]Balaamu akamwambia punda; Kwa sababu umenidhihaki; laiti ningekuwa na upanga mkononi mwangu ningekuua sasa hivi.

[30]Yule punda akamwambia Balaamu, Je! Mimi si punda wako, nawe umenipanda maisha yako yote hata leo? Nimezoea kukutenda hayo? Akasema, La!

[31]Ndipo BWANA akafunua macho ya Balaamu akamwona malaika wa BWANA amesimama njiani, ana upanga mkononi mwake, umekwisha kufutwa naye akainama kichwa, akaanguka kifudifudi.

[32]Malaika wa BWANA akamwambia, Mbona umempiga punda wako mara tatu hizi? Tazama mimi nimekuja ili kukupinga, kwa sababu njia yako imepotoka mbele zangu,

Hii ikiomyesha kuwa Mungu hafurahishwi pale tunaposhindwa kuwaonea huruma wanyama, ikiwa kama Mungu anawatuza kwanini na sisi tushindwe, kiufupi tabia ya kutesa wanyama Mungu hafurahishwi nayo, ikiwa kama tunaishi nao na hatupo madhara yoyote basi tuwajali na tuwalinde, kupitia kufanya hivi kuligana na maandiko neno la Mungu linasema kinatuongezea siku nyingi nza kuishi duniani

Kumbukumbu 22:6 “Kiota cha ndege kikitukia kuwa mbele yako njiani, katika mti wo wote, au chini, chenye makinda au mayai, naye koo ameatamia juu ya makinda, au juu ya mayai, usimtwae yule koo pamoja na makinda;

7 sharti umwache yule koo aende zake, lakini makinda waweza kuyatwaa uwe nayo; ili upate kufanikiwa, ufanye siku zako kuwa nyingi”.

Basi tujitahidi kuishi vizuri na wanyama wetu ikiwa wanaishi nasi vizuri, basi haina haja ya kuwapiga ovyo ovyo

Mungu akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *