Adhama maana yake ni ‘uzuri wa hali ya juu sana’. Uzuri huu wa hali ya juu upo kwa Bwana Yesu peke yake, hakuna mtu wala kiumbe chochote chenye uzuri wa hali ya juu kama alivyo Bwana Yesu
Zaburi 93:1[1]BWANA ametamalaki, amejivika adhama, BWANA amejivika, na kujikaza nguvu. Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
Kuna vifungu kadhaa katika Biblia vinavyozungumzia neno hili, ‘adhama’.
Zaburi 96:6
[6]Heshima na adhama ziko mbele zake,
Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
Zaburi 104:1
[1]Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Wewe, BWANA, Mungu wangu,
Umejifanya mkuu sana;
Umejivika heshima na adhama.
Isaya 33:21
[21]Bali huko BWANA atakuwa pamoja nasi, mwenye adhama; mahali penye mito mipana na vijito, pasipopita mashua na makasia yake; wala hapana merikebu ya vita itakayopita hapo.
2 Wakorintho 4:7
[7]Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili adhama kuu ya uwezo iwe ya Mungu, wala si kutoka kwetu.
Vifungu vingine vinavyotaja neno hili ni
1 Mambo ya Nyakati 16:27
[27]Heshima na adhama ziko mbele zake;
Nguvu na furaha zipo mahali pake.
Zaburi 21:5
[5]Utukufu wake ni mkuu kwa wokovu wako,
Heshima na adhama waweka juu yake.
Zaburi 113:3
[3]Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la BWANA husifiwa.
Zaburi 148:13
[13]Na walisifu jina la BWANA,
Maana jina lake peke yake limetukuka;
Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
Zaburi 29:4
[4]Sauti ya BWANA ina nguvu;
Sauti ya BWANA ina adhama;
Kutokana na vifungu hivyo, Yesu pekee ndiye mwenye heshima na adhama yote hakuna mwingne anayestahili kupewa…
Ufunuo wa Yohana 5:9
[9]Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Maran atha
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.