Waitwao ‘waoga’ ambao hawataurithi uzima wa milele ni watu wa namna gani (ufunuo 2:18)

Maswali ya Biblia, Uncategorized No Comments

Bwana Yesu asifiwe, karibu tena tujifunze Neno la Mungu kama maandiko matakatifu yanavyosema katika zaburi 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Kuligana na swali letu ili tuweze kuelewa zaidi tusome kwanza kifungu hiki

Ufunuo 21:8 “BALI WAOGA, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.

Hapa maandiko yanaeleza kuwa waoga, wasioamini nk.. sehemu yao ni katika ziwa la moto.

Waoga ni watu wa aina gani sasa?

Waoga ni watu mwenye hofu, na hali hii usababishwa na kupungukiwa na uhakika jambo fulani kama litafanikiwa, mfano mzuri tumzungumzie mwanafunzi ambaye anafanya mtihani, pale anapowaza kuwa huu mtihani nafanya lakini sijui kama nitafahulu, kwa kufanya hivyo tu moja kwa moja huyo mwanafunzi tayari hofu ipo ndani yake, kwa sababu hana uhakika kama ataweza kufanya vizuri. Hata kwa mtu anayewaza kesho itakuwaje, atakula nini atavaa nini, ataishije naye ni mmoja ya watu wenye hofu, ambao Mungu hapendezwi nao, hata kwa mtu ambaye hana uhakika kama siku akifa atakwenda wapi huyo pia naye hofu ipo ndani yake kwa kukosa tu uhakika wa maisha yake. Sasa haya yote mbele za Mungu ni machukizo ndiyo maana anasema watu kama hao sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo mto.

SASA TUTAWEZAJE KUSHINDA HALI HII YA WOGA NDANI YETU:

Tusome

Warumi 8:14-17

[14]Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

[15]Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo HOFU; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

[16]Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

[17]na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

Hapo maandiko yanatueleza hakuna njia pekee ambayo itaweza ondoa hali hii zaidi ya Yesu peke yake, msaada huu inatokea pale tunapomwamini na kumfanya awe Bwana na mwokozi wa maisha yetu hapo ndipo ile nguvu ya KUSHINDA inaingia ndani yetu, na Roho wa Mungu anakuwa ndani yetu, kwahiyo yale mashaka yote, woga wote, hofu zote zinaondolewa za kuwaza kesho tutakula nini, kesho itakuwaje, je kweli nikifa nitaenda mbinguni sasa haya yote yanaondolewa na ujasiri unakuwa ndani yetu.

Maana mambo haya yanakuwepo ndani ya mtu pale tu anapokuwa nje ya Kristo

1Yohana 4:18

“Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo”.

Jitazame maisha yako je? mashaka, yapo kwako, woga upo kwako hofu ipo kwako, kama hali hizi bado zipo ndani yako tambua kabisa Yesu hatupo ndani yako unapaswa kufanya maamuzi mapema ili hii hali ya kuishi pasipo kuwa na Imani kuwa Mungu atafanya

2Timotheo 1: 7 “ Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi”.

Kingine pia kama neno la Mungu linavyotueleza hapo tunampokea Kristo anatuondolea roho ya woga, na zaidi anatupa nguvu ya upendo na moyo wa kiasi, hii nguvu inapokuwa imeingia ndani, kutokana na hofu za maisha kuna wakati mwingine unaweza pelekea kufanya mambo maovu ilamradi tu upate kitu kitakacho weza kukusaidia kumudu hali unayopitia mfano unakuta mtu anakupokea rushwa, au anasema uongo ili apate jambo lake, au anafanya uzinzi ili akidhi hitaji lake, sasa haya yanaondoka pale moyo wa kiasi unapokuwa ndani ya mtu, kwahiyo hakikisha kabisa huwi mbali na NEEMA HII YA WOKOVU maana inatupa KUSHINDA MAMBO MENGI NA KUFIKIWA ZILE AHADI ZA MUNGU

Marko 4.39 Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.

40 Akawaambia, MBONA MMEKUWA WAOGA? Hamna imani bado?

41 Wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, Ni nani huyu, basi, hata upepo na bahari humtii?

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *