NINI MAANA YA KUHUTUBU?’

Maswali ya Biblia No Comments

Neno KUHUTUBU chanzo chake ni HOTUBA , Hotuba ni maneno yaliyoandaliwa na mtu kwa ajili ya kuyazungumza mbele ya mkutano au kusanyiko la watu. Kitendo cha kutoa hotuba ndicho kinajulikana kama KUHUTUBU. Maneno ya hotuba yanaweza kuwa ya kimaendeleo au ya kimkakati.

Kuna tofaut kubwa ya kuhutubu kawaida na kuhutubu kibiblia , watu wa ulimwengu wanahutubia mikakati ya kiulimwengu kwa maneno yao wenyewe lakini watu wa Mungu wanahutubia maneno ya Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu.Mfano viongozi wa kisiasa huandaa hotuba zao kulingana na jambo linaloizunguka jamii waliyopo. Wachungaji na waalimu huandaa hotuba kulingana na neno la Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu, wanahutubu maneno ya Mungu

 1 Timotheo 5:17
[17]Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.

Wazee watawalao vema na wahesabiwe kustahili heshima maradufu; hasa wao wajitaabishao kwa kuhutubu na kufundisha.

   Matendo ya Mitume 20:7[7]Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu, akiazimu kusafiri siku ya pili yake, naye akafuliza maneno yake hata usiku wa manane.

Lakini pia kuna watumishi wa Mungu wenye karama ya kinabii wanaposimama mbele ya mkutano na kutoa unabii, kuwajenga watu na kuwapa tumaini juu ya mambo yajayo nao pia wanahutubu

1 Wakorintho 14:4-5
[4]Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.


[5]Nami nataka ninyi nyote mnene kwa lugha, lakini zaidi sana mpate kuhutubu, maana yeye ahutubuye ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha, isipokuwa afasiri, ili kusudi kanisa lipate kujengwa.

Hapo inazungumziwa hotuba ya kutoa unabii au kwa lugha ya kingereza ‘to prophecy’

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *