Waanaki ni akina nani kama tuwasomavyo katika biblia?

Maswali ya Biblia No Comments

Ukisoma katika kitabu cha yoshua watu hawa wametajwa

Yoshua 15:13
[13]Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, maana ni Kiriath-arba, ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki (huo ndio Hebroni).

Waanaki walikuwa jamii ya watu warefu na wakubwa waliotoka  katika uzao wa mtu mmoja  anayeitwa  anaki mtoto wa Arba sawa na andiko hilo hapo juu
Na maana halisi ya jina hilo kutokana na lugha ya kiyahudi linalomaanisha
MTU MREFU NA MWENYE SHINGO NDEFU, na watu hawa waliishi upande wa kusini mwa israeli, hawa walikuwa watu wenye nguvu sana, na walikuwa hodari sana katika vita kiufupi walikuwa watu  tofauti sana na watu wengine waliokuwako kipindi hicho, maana hakuna mtu aliyeweza kushindana nao

Baadhi ya maandiko yameeleza kuhusu watu hawa
Tusome

Kumbukumbu la Torati 9:1-3

[1]Sikiza, Ee Israeli; hivi leo unataka kuvuka Yordani uingie kwa kuwamiliki mataifa yaliyo makubwa, na yenye nguvu kukupita wewe, miji mikubwa iliyojengewa kuta hata mbinguni,

[2]watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?

[3]Basi jua siku hii ya leo kuwa BWANA, Mungu wako, ndiye atanguliaye kuvuka mbele yako kama moto uteketezao; atawaangamiza, tena atawaangusha mbele yako; ndivyo utakavyowafukuza na kuwapoteza upesi, kama alivyokuambia BWANA.

Kumbukumbu la Torati 1:28

[28]Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki.

Yoshua 21:11

[11]Nao wakawapa Kiriath-arba, huyo Arba alikuwa baba yake Anaki, (ndio Hebroni), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na malisho yake yaliyouzunguka pande zote.

Lakini wayahudi kuligana na tamaduni zao waliamini kuwa hawa waanaki chimbuko lao limetoka katika uzao wa wanefili yaani majitu, waliokiwepo kabla ya gharika kutokea, habari hii tunaisoma katika kitabu cha mwanzo  6:4, pia tukisoma hata katika habari  1samweli tunaona pia watu hawa wanaoneka,  yule goliathi

kwanini sasa Mungu aliruhusu watu hawa wakubwa kuliko wanadamu wengine wawepo, kwanini asingetuumba watu wa aina moja tu? JE KIROHO TUNAJIFUNZA NINI?

Mungu alikuwa na uwezo wa muumba watu wa aina moja tu, lakini mpka anaumba watu kama hao, lipo jambo la kujifunza hapa, hata kiroho  wapo watu wakubwa majitu ambao wanapambana kuhakikisha wanashinda nasi ili tuweze kukwama katika safari hii ya kwenda mbinguni na lengo kuu la hawa watu maishani huwa kwa ajili ya kuleta vitisho, lakini kama watu wa Mungu walivyoweza kushinda hata nasi pia tunaweza kuwashinda hwa majitu,

Na tutawezaje kuwashinda, nguvu pekee inayotupa ushindi ni kimkabidhi Bwana wetu Yesu Kristo maisha yetu sawa sawa maandiko yanavyotumbia (warumi 10:9)
pale tunapomwamini na kukamilisha hatua zote za wokovu hapo ndipo ile nguvu ya kushinda inakuwa ndani yetu, hata jambo lolote litakapo inuka kwa ajili ya kukushusha au kukutisha kwa kuwa  tayari Yesu yupo ndani yako  lazima utashida tu,  maana hata tukisoma hata habari ya daudi na goliathi, jambo kimwonekano daudi alionekana mdogo na goliathi alionekana mkubwa haikumfabya daudi hashindwe vita hiyo, na kitu kilichomfanya daudi ashide ni kwa sababu alimwamini Mungu kuwa atamshindia, na ikawa hivyo hata kwa sisi watakatifu tunapopitia jambo lolote lazima tuamini kuwa Mungu ametushindia.

Lakini ni rahisi mtu kuanguka, na kuangamizwa au kutishwa ikiwa kama utakuwa nje ya Kristo, ushindi wako na ujasiri wa kuweza kushinda hali zozote ile kitu cha ni wewe kumpokea tu ndani ya moyo wako ili uwe salama.

Ubarikiwe sana

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *