Wanazorayo ni madhehebu gani katika maandiko? Matendo 24:5

Maswali ya Biblia No Comments

Kipindi Bwana Yesu yupo hapa duniani kulikuwa na madhehebu mawili tu katika uyahudi ambayo yalikuwa Mafarisayo na Masadukayo

Matendo 5:17 “Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu,”

Tukisoma na matendo 15 inawaelezea Mafarisayo tusome

Matendo 15:5 “Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika torati ya Musa”.

Madhehebu haya ndiyo yaliyokuwako kipindi Bwana Yesu yupo, na yote yalikuwa yanaamini torati ya Musa, lakini katika swala la kiama hapa ndiyo walitofautiana imani, maana Masadukayo hawakuamini kama kuna ufufuo lakini Mafarisayo wao waliamini kuwa ufufuo upo

Mathayo 22:23

[23]Siku ile Masadukayo, watu wasemao ya kwamba hakuna kiyama, wakamwendea, wakamwuliza

Lakini baada ya Yesu kuondoka, hapo ndipo lilizaliwa dhehebu lingine lililoitwa Wanazarayo, nalo pia liliamini torati ya Musa sema hili lilizama zaidi kwa kuamini kuwa Yesu aliyetokea Nazareti ndiye masihi

Matendo 24:5 “Kwa maana tumemwona mtu huyu mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazorayo”.

Ukisoma tena

Mathayo 2:23 “akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.”

Na dhehebu hili liliitwa hivyo kwa sababu ya mji wa Nazareti, sehemu ambayo alilelewa, kwahiyo mtu yeyote aliyekuwepo mahali pale aliitwa Mnazorayo

JE MADHEHEBU HAYA YALIFANIKIWA KUMJUA KRISTO YESU.?

Mitume wa Bwana Yesu, hawakuwa wafuasi wa dhehebu lolote kipindi kile, na pia hata ile siku ya pentekoste Roho Mtakatifu hakushuka katikati ya haya madhehebu,

bali siku ile Roho alishuka kwa watu ambao tayari wamefanyika wanafunzi wa Yesu ambao waliweza kusikia maagizo ya Bwana Yesu na kuyatenda walipofundishwa, kwahiyo Roho hakushuka katika dini, bali kwa hawa wote waliokuwa wanafunzi

Na jambo hili hata leo ndivyo linavyofanyika Roho Mtakatifu hashuki katika dini fulani au dhehebu fulani, hata kama liwe zuri kiasi gani kama hakuna wanafunzi wa Yesu , watu wanaotii maagizo ya Bwana wetu Yesu Kristo kamwe hawezi kushuka Roho wa Bwana lakini anashuka kwa watu ambao wamekubari kutii Sheria ya Bwana na kuifuata, hivyo usitishwe na ukubwa wa kanisa lakoz au umaarifu wa dini yako bali tazama JE wewe ni mwanafunzi wa Yesu ili yule Roho ashuke ndani yako maana hii ndiyo AHADI tuliyopewa na Bwana wetu Yesu Kristo

Basi ikiwa bado ujampokea Yesu Kristo maisha mwako basi wakati ni sasa mwamini awe Bwana na Mwokozi wa Maisha yako, kisha ufuate maagizo ya Bwana ili yule Roho Mtakatifu ambaye ndiye masaidizi aingie ndani yako

Yohana 14:24-26

[24]Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka.

[25]Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu.

[26]Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Maran atha

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *