Elewa Tafsiri ya 1 Wakorintho 8:8 lakini chakula hakituhudhurishi mbele Za Mungu.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Tafsiri ya neno “kutuhudhurisha” maana yake ni “kutusogeza karibu na jambo fulani au kitu fulani .”

Maana yake ni kwamba chakula sisi tunachokula tunachokula na kinaenda kutupa nguvu katika miili yetu hakitusogezi karibu na Mungu wala kutuweka mbali na Mungu la!.

Huwezi kula chakula kingi au mboga mbali mbali halafu ndio zikufanye uwe karibu na Mungu sivyo hivyo. Hebu tusome.

1Wakorintho 8:8 “Lakini chakula hakituhudhurishi mbele za Mungu; maana, tusipokula hatupunguziwi kitu, wala tukila, hatuongezewi kitu.

9  Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu”.

Si kwamba ukila chakula fulani ndio kitakusogeza karibu na Mungu au kitakufanya uwe najisi kwa Mungu la!,

Kitu pekee kinachotuweka mbali na Mungu ni dhambi tu na kinyume chake kinachotusogeza karibu na Mungu ni kumuamini Yesu Kristo lakini pia na kuishi maisha matakatifu yaani kujiepusha na maovu.

Isaya 59:1 “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;

2 lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusiki”

Unaona hapo!, kumbe ni dhambi peke yake tu!,
Hivyo tukila nyama ya swala,punda,fisi,konokono,nguruwe,mnafu,ng’ombe ,mbuzi,twiga,nk vyote hivyo havituhudhurishi mbele za Mungu. Maaana yake ni kwamba hakituongezei kitu wala kutupunguzia kitu rohoni tunapokula ama tusipokula!

Sasa vipi kuhusu kunywa sumu,bangi,pombe,ni sahihi kuyatumia kama mboga mboga tu? Maana kama yanaomekana hayana madhara je? Ni sahihi kutumia maana havituhudhurishi mbele za Mungu!?.

Sasa tukianza na pombe, pombe yoyote ile maadam inaitwa pombe ina kilevi ndani yake ambayo hupelekea kuleta Mafarakano,ugomvi, utamanifu yaani uasherati na uzinzi pombe inachochea mambo kama hayo.na mengine mengi ambayo hayo ni machukizo makubwa mbele za Mungu.

Pia bangi si sahihi kuitumia maana mtu anapotumia inamtoa katika hali yake ya kufikili kwa kawaida kama mwanadamu.
Hivyo bangi inaharibu akili ya mtu huyo.
Na si hivyo tu inamfanya anakuwa ni najisi mbele za Bwana.

Kama maandiko yanavyosema…

Mathayo 15:19 “ Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;

20  hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi”

Hivyo mawazo yale yanayotoka moyoni mwake yanamfanya anakuwa najisi mbele za Bwana.

Hivyo si vitu vyema kama pombe nk maana vinachochea mambo mabaya mbele za Mungu.

Waefeso 5:17  “Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

18  Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho”

Kama maandiko yanavyosema tusiwele kwa mvinyo(wine/pombe) bali tujazwe Roho ndani yetu. Maana ndio tutatembea katika mapenzi ya Bwana wetu!.

Hivyo vyakula ambavyo havitufanyi kutoa mambo mabaya mioyoni mwetu basi hivyo tunaweza kuvitumia. Kabisa

Kama chakula hakituhudhurishi mbele za Bwana vipi kuhusu meza ya Bwana? Maana maandiko yanatwambia kile chakula tunapokila tunaitangaza mauti ya Bwana hata atakapokuja.

Meza ya Bwana hilo ni Agizo alilolitoa Bwana kama vile ubatizo tu jinsi ulivyo hivyo mkate ule tunajua wanashiriki watu pia hata wakiwa majumbani mwao maana kinapokuwa katika mazingira ya kiibada hicho kinaonekana kama chakula tu maana ni chapati tu ile.watu wananunua ama kuandaa hata wapagani wanaandaa na kula hatuwezi kusema pale wanaitangaza mauti ya Bwana kwani kile nichakula tu.

Sasa mkate huo huo unapotumika katika ibaada yaani katikati ya waaamini hicho katika roho ni mwili wa Kristo unakuwa umsbadilika na hata ile divai inakuwa sio divai tena inapotumika katika ibada bali inakuwa ni damu ya Bwana Yesu halisi kabisa itupayo uzima katika roho zetu.

Kama vile tu maji yale ya kubatizia maji mengi yanatumika pia kwa kunyweshea ng’ombe, mbuzi na kuoga pia Hauwezi tukasema ng’ombe anapokunywa ama mbuzi au tunapoyaoga basi tunakuwa tumebatizwa la!

Vivyo Vivyo ngano/divai inapokuwa kwa matumizi nje na ibada inakuwa ni chakula kama chakula tu na hakituhudhurishi mbele za Bwana.

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *