Fahamu maana ya Muhubiri 6:3 heri mimba iliyoharibika kuliko huyo.

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Mstari huu ukiusoma kwa makini unatufundisha mambo makuu mawili ambayo Kuna makundi mawili ya watu walioko hapa duniani. Na tutaangalia kundi moja baada ya lingine.

Kundi la kwanza ni kundi la Watakatifu.

Hili ni kundi la watu lililomuamini Yesu Kristo au lililoamua kuyasalimisha maisha yake kwa Mungu. Ni watu ambao hawaishi kwa kuifata kawaida ya ulimwengu kwa kujizuia mambo maovu na kuishi kwa kumpendeza Mungu katika Kristo Yesu.

Ni watu waliojikana nafsi zao kweli kweli yaani kuacha mambo wanayopendwa na ulimwengu ambayo ni machukizo mbele za Mungu na watu wa namna hii wanaishi kam wapitaji tu katika ulimwengu huu.

Kama vile Ibrahimu alivyoishi kama mpitaji akiitazamia ahadi ya Mungu,  ijapokuwa alikuwa na maisha mazuri na alikuwa ni Tajiri lakini hakuvutiwa na mambo ya ulimwengu huu kama vile Luthu.

Waebrania 11:[9]Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.

[10]Maana alikuwa akiutazamia mji wenye misingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Lakini si Ibrahimu tu lakini pia Mitume wote, manabii wote na akina Musa,Yohana Mbatizaji.nk waliishi kama wapitaji tu hapa duniani. (Waebrania 11:23-40).

Hawa waliishi kama wapitaji tu wala hawakuangalia ulimwengu unasemaje juu yao walihesabu wao ni kama kondoo wapelekwao machinjioni.
Na sisi kama Wakristo katika nyakati hizi za Mwisho hatuna budi kuishi kama hawa watu.
Tuishi kama watu tusiokuwa na fungu lolote hapa duniani hii itatusaidia kupiga mbio kwa wepesi zaidi hapa duniani.

Kundi la pili:

Hawa ni watu ambao wamechagua fungu lao kuwa hapa hapa Duniani ambalo linakuwa na uzo mkubwa na utajiri mwingi linaheshimiwa na watu wengi lakini mpaka linakufa linakuwa halijaridhika na kitu chochote bado.

Linakuwa na kiu ya mambo ya ulimwengu huu isiyokoma na mwisho wake ni mauti ya milele.

Sasa Sulemani anasema kundi la namna hii hali heri popote maana hapa duniani limetafuta kwa nguvu nyingi sana na kwa maumivu makali na bado linakufa likiwa halijafaidi lakini pia hata kule nga’ambo linakwenda kupata hasara na ndio maana Sulemani anasema ni heri mimba ya watu wa namna hii ingeharibika maana ni hasara tu.

Ukisoma juu yake pia anasema…

[2]mtu aliyepewa na Mungu mali, ukwasi, na heshima, hata asipungukiwe na kitu cho chote kwa nafsi yake, katika yote anayoyatamani walakini Mungu hamwezeshi kula katika hizo; bali mgeni hula. Hayo ndiyo ubatili hasa, nayo ni ugonjwa mbaya.

Kama maandiko yanavyosema kuwa tujiwekee hazina mbinguni. Ikiwa Mungu kakubariki kwa kikubwa ama kwa kidogo ni heri ukakiwekeza kwake pasipo kujali chochote ukijua kabisa unahompa Mungu hakipotei kamwe kitarudi tena na zaidi.

Hazina inayozungumziwa hapa sio ya miaka 10 mbele au miaka 5 mbele la ni hazina ya maisha yote kana na kwamba ni ya milele/kama mtu ataishi maisha ya milele hapa duniani  hiyo ndio inayosabaisha kutokuridhika!,uchoyo,ubinafsi nk
Hivyo sisi watu wote tuliookoka hazina yetu inabidi iwe kwa Mungu wetu tusiwe kama watu wa Dunia hii!

Maranatha.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *