Tafsiri ya ndoto KUOTA UPO KANISANI NI HII

Ndoto 2 Comments

Bwana Yesu asifiwe. Karibu tujifunze Biblia

Kwanza kabisa kanisa ni hekalu au nyumba ya Mungu. Hivyo ni wazi kwamba hii ni ndoto njema itokayo kwa Mungu, Shetani hawezi sababisha ndoto ya namna hii.
Ndoto hii Huweza kuleta maana mbili, Ikiwa Umeokoka na umesimama imara basi Mungu anakuonesha upo katika njia sahihi kabisa Ambayo ni kuwa uweponi au Nyumbani mwake, Na uendelee kumtafuta kwa bidii. Ndio Maana Daudi anasema…..

Zaburi 122:1
” Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana.”

Lakini iwapo umeota ndoto hii na unajijua hauna Mahusiano mazuri na Mungu wako kwa matendo yako ya dhambi, Basi huo ni wito na haupaswi kupuuziwa, Maana ni Mungu anakwita uweponi mwake Sababu hakika wewe SI wa Ulimwengu huu.

Mungu huzungumza na Watu wake kwa njia mbalimbali hata zaidi ya mara moja

Soma….

Ayubu 33:14-15
14″ Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.

15 Katika NDOTO , katika MAONO YA USIKU, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;”

Mpendwa inakupasa utii sauti hiyo maana hujui kwanini imekuja kwako Leo, hapa duniani sisi tu wapitaji kesho unayoingojea inaweza isiwe yako, Tubu Leo kwa kudhamiria kuziacha dhambi zako, na uachane na Ulimwengu huu moja kwa moja.
Pengine umeshasikia wito huu zaidi ya mara moja kuhusu kutubu na kuziacha njia zako Za dhambi, Fanya maamuzi sahihi ukomboe roho yako usiifanye shingo yako kuwa Ngumu.

Haijalishi hata kama wewe ni muislam siyo kigezo cha kukataa wito wa Mungu kwa maana amekuchagua,Anza na uamuzi wa kufungua somo la
KUONGOZWA SALA YA TOBA
na Mungu atafanya Yale yaliyosalia

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

2 thoughts on - Tafsiri ya ndoto KUOTA UPO KANISANI NI HII

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *