NOVENA NINI, je ipo katika Biblia ?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno hili novena chimbuko lake limetoka katika lugha ya kilatini linaandikwa “Novem” ikiwa na maana ya tisa(9).
Na baadhi ya madhehebu mfano katoliki na Orthodox, wamelichukua neno hili na kulitumia katika aina fulani za sala ambazo ni mfufulizo Kwa kipindi cha siku tisa

Na sala hizo huwa kwaajili ya kuomba jambo fulani au kushukuru kwa kipindi cha siku 9 mfufululizo, na ibada huwa zinahusisha ibada za kuomba Rozari kwa Wakatoliki, ambapo jambo hili si sahihi kibiblia wala si agizo la Mungu watu wasali Rozari

Sasa msukumo wa kuomba Novena, (yaani siku 9) mfululizo umetokana na matukio maalumu yanayotokea baada ya siku 9, au miezi 9 kumalizika. Kwamfano utaona kabla ya Pentekoste kutimia, walikusanyika Mitume na watu wengine baadhi mahali pamoja kuomba, na wakaomba kwa muda wa siku 9, baada ya Bwana Yesu kupaa na siku ya 10 ikawa ni Pentekoste.

Hivyo jambo hili la kupokea Roho Mtakatifu baada ya Maombi likawa limeaminika na madhehebu hayo kuwa ni lazima liendelee ili kupokea jambo lingine kutoka kwa Mungu, mfano wakaangalia hata kwa wamama wajawazito nao hupokea jambo jipya baada ya miezi tisa, Sasa jambo hili viongozi wa madhehebu haya likawafanya wakaamini kuwa katika 9 kuna siri au kitu katika 9 (novena)

Lakini swali la kujiuliza Je katika maandiko (biblia takatifu) ni kweli imetuagiza kufanya jambo hili yaani kuwa na maombi ya novena
katika maombi ili kupokea jambo maalumu kutoka kwa Mungu? Kwamba tuwe na maombi maalumu ya kurudia rudia kwa muda wa siku 9 ili tupokee jambo kutoka kwa Mungu?

Hapa kukuna ukweli wowote, na Wala jambo hili halipo katika Biblia pia si maagizo ya Mungu, hata tukisoma maandiko ile siku ya pentekoste, tunaona kabla ya Pentekoste walikuwa wamekusanyika mahali pamoja wakisali, wakimwomba Mungu na Mariamu mama yake Yesu alikuwemo miongoni mwao, naye pia akimwomba Mungu, na hawakuwa na sanamu ya mtakatifu Fulani aliyetangulia kufa!, bali walikuwa wakimwomba Mungu aliye juu, (Matendo 1:12-14)

Hivyo jambo hili si la Ki Mungu wala hakutuwekea tuwe na kipindi fulani cha siku 9 maalumu ili tuweze kupokea jambo fulani kutoka kwake, Utaratibu huu umetengenezwa na wanadamu, kufuatia ushawishi wa siku ya Pentekoste. Hivyo kama umetengenezwa na wanadamu, hauwezi kuwa Sharti, au Agizo la lazima kwa wakristo, kwamba usipofanya hivyo ni kosa kibiblia!.

Agizo hili linaweza kuwa la binafsi, kama tu vile mfungo usivyokuwa sharti, ni jinsi mtu atakavyosukumwa na kuongozwa kufunga!.

Maana ndani ya Sala hizi, zimehusishwa na Ibada za sanamu, jambo ambalo ni chukizo mbele za Mungu, kuweka kisanamu cha Mtakatifu fulani, hii si sawa maana hata Ile siku ya pentekoste tunaona walipokuwasanyika walikuwa katika kuomba tu Wala hakukuwa na sanamu ya aina yoyote, hii ikithibitisha kuwa jambo hili si la Mungu.

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Novena haipo kibiblia,..kama mtu atajiwekea utaratibu wake binafsi wa kusali Novena, na sala hiyo ikawa ni kulingana Neno la Mungu, isiyohusisha sanamu wala desturi za kipagani basi hafanyi dhambi!, huenda ikawa bora kwake.

Lakini inapogeuka na kuwa sharti, na tena ikahusisha ibada za sanamu basi inakuwa ni machukizo makubwa mbele za Bwana kulingana na maandiko

Bwana akubariki.
Kwa Msaada waweza Wasiliana nasi Kwa namba hizi

+225693036618/ +225789001312

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya mfundisho ya NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *