MAKANDA NI NINI?

  Maswali ya Biblia

Jina la Bwana wetu Yesu kristo litukuzwe . Karibu mwana wa Mungu katika kujifunza Neno la Mungu

Je makanda ni nini?

Makanda ni kwa jina /neno jingine ni (KAPU). Ambacho hutumika kuweka au kubebea vitu tofauti tofauti sana sana vyakula au nafaka.

Katika maandiko Neno hili unaweza ukakutana nalo katika vifungu kadha wa kadha, mfano wa vifungu hivyo ni:

Mathayo 15:37

[37]Wakala wote wakashiba; wakayaokota masazo ya vipande vya mikate makanda saba, yamejaa.

Marko 8:8

[8]Wakala, wakashiba, wakakusanya mabaki ya vipande vya mikate makanda saba.

Luka 16:6-7

[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini.

[7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.Luka 16:5-7

[5]Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu?

[6]Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini.

[7]Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini.

Ni nini tunapaswa kujua na kujifunza juu ya makanda ya mikate waliyoyakusanya na wanafunzi wa Yesu ambayo baadaye waliyosahau mpaka wakaanza kulalamikiana na kulaumiana..Hadi Yesu akawakemea..(Marko 8:14-21)

Ni kwamba waliweka mioyo yao katika makapu yao, katika hazina zao, hata waliposahau wakapaniki.

Na hali hii pia ipo miongoni mwetu sisi, tuliookoka. Tunafikiri sana makapu yetu yana nini, kwa miezi 10 mbele, kwa miaka 3 ijayo..na pale tunapopungukiwa na kukosa hata uhusiano wetu na Mungu unakufa..Lakini Bwana wetu Yesu kristo anatuambia tusiwe mashaka , wala tusiyasumbukie hayo..bali tuutafuta kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine atatuzidishia..kwasababu maisha ni zaidi ya chakula.

Bwana akubariki.

Tafadhali shea na wengine ujumbe huu;

Pia Kwa maombezi/ Ushauri/ Maswali/ Whatsapp:
Tuandikie katika BOXI la Maoni hapo chini au
Piga namba hizi: +255693036618 au +255789001312

LEAVE A COMMENT