GOMBO NI NINI, katika Biblia ?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana wetu Yesu Kristo atukuzwe,
Karibu katika kujifunza maneno ya uzima

Gombo ni aina ya vitabu ambavyo vipo katika namna ya kuviringishwa, kwa lugha ya kiingereza vinatambulika kama “Scrolls”

Aina ya hii ya vitabu ilitumika sana katika karne za nyuma na vilikuwa ni vitabu vya aina ya ngozi.

Lakini kwa wakati wetu wa sasa havitumiki tena , hii ni kutoka na kuongezeka kwa maarifa duniani.

Vitabu vinavyotumika sasa, vinatengenezwa kwa namna ya makaratasi, na vinakuwa na kurasa..Lakini Gombo havikuwa na kurasa, bali ni ngozi iliyokuwa na maandishi na kuviringishwa.

Mfano wa kitabu cha Gombo ni vile tunavyovisoma katika kitabu cha Ezekieli na Ufunuo.

Katika kitabu cha Ufunuo, tunasoma Bwana wetu Yesu Kristo akikipokea kile kitabu chenye mihuri saba. Sasa kitabu hicho ni cha aina tofauti si kama vitabu vya wakati wa sasa vyenye kurasa la! bali kilikuwa ni gombo, yaani kitabu kilichoviringishwa, na vitabu hivi vya kuviringishwa ndivyo vilivyokuwa vinafungwa kwa mihuri.. vilikuwa vinafungwa kama vile shati linavyofungwa kwa vifungo vyake,

Kwahiyo mahali popote katika biblia takatifu panapotajwa neno kitabu, palimaanisha aina hiyo ya kitabu (yaani Gombo)..na haikumaanisha aina ya vitabu tulivyo navyo kwa wakati wa sasa.
Katika biblia Unaweza kulipata neno hilo Gombo , kupitia mistari ifuatayo. Zaburi 40:7, Yeremia 36:2-6, Ezekieli 2:9, Ezekieli 3:3, Zekaria 5:1-2, na Waebrania 10:7.
Kwa msingi huo wa kuelewa nini maana ya Gombo, utatusaidia kuelewa vizuri juu ya MIHURI SABA ya kitabu cha ufunuo.
Kama utapenda kujua juu ya ufunuo wa Mihuri saba unaweza Wasiliana nasi Kwa namba hizo chini kisha tukakutumia somo hilo.
Je umempokea Yesu?, je Umebatizwa ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa jina la Yesu?, Je umepokea Roho Mtakatifu a unaishi maisha matakatifu ya kumpendeza Mungu?.


Kumbuka Bwana yupo mlangoni, na unyakuo wa kanisa ni siku yoyote.
Maran atha!
Tafadhali washirikishe na wengine habari hizi njema,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *