Maana ya Adamu kibiblia?

  Maswali ya Biblia

Shalom, karibu tujifunze neno la Mungu.

Maana ya neno Adamu ni “wa udongo” (kwa kiebrania) yaani mtu aliyetokana na udongo.

Kama ni msomaji mzuri wa biblia utakumbuka mwanadamu wa kwanza kuumbwa alipewa jina na Mungu mwenyewe na jina ilo ndiyo Adamu.

Mungu alimwita jina Adamu kutokana na asili ya alipotolewa, yaani mavumbini/ardhini.

Tusome..
Mwanzo 2:7 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai.

Na jina hili hakupewa mwanaume tu, bali Mungu aliwaita wote mwanaume na mwanamke, Adamu yaani “wa udongo”

Tusome..
Mwanzo 5:1 Hiki ndicho kitabu cha vizazi vya Adamu. Siku ile Mungu alipoumba mtu, kwa sura ya Mungu alimfanya;

[2] mwanaume na mwanamke aliwaumba, akawabariki akawaita jina lao ADAMU, siku ile walipoumbwa.

Hivyo watoto wote waliofuata baada ya Adamu, wakaitwa Wana-damu ( yaani wana wa aliyetokana na udongo) kwaiyo na sisi sote asili ya miili yetu ni ardhini, na ndio maana tunakufa.

Tusome..
Mhubi 3:20 Wote huenda mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena.

Lakini kumbuka kuna maisha baada ya kifo, maisha ya mbinguni, maisha ambayo hatutaishi tena kama Wana-damu, tukioa na kuolewa, tukila na kunywa, bali tutaishi kama malaika mbinguni kwa maana tutapewa miili mingine isiyo ya udongo.

Tusome..
Marko 12:25 Kwa maana watakapofufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali huwa kama malaika walioko mbinguni.

Je! na wewe ni mmoja wao watakaovikwa miili mipya ya utukufu na kufanana na malaika mbinguni?

Kumbuka tumaini ilo lipo kwa mmoja tu, Yesu kristo, Bwana na mwokozi wa maisha yetu pamoja na miili yetu, wala hakuna tumaini kwa mwingine awaye yote chini ya mbingu.

Matendo ya mitume 4:12 Wala hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuolewa kwalo.

Bwana akubariki

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushare…

Au wasiliana nasi kwa namba hii 255693036618

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

LEAVE A COMMENT