Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo
Maana ya kuota ukiwa unapigana kunaweza kubeba maana mbili aidha upo katika mashindano au upo katika vita!
Tuziangalie maana hizi mbili kwa ufupi
1. KUWA KATIKA MASHINDANO
Mashindano huja kwa Hali Ambayo watu wanapogombania kitu chenye THAMANI Fulani ambapo Kila mtu anataka akipate yeye, kunaweza kuwa thawabu, madini,fedha,kazi, mapenzi n.k
Katika biblia Tunamwona mtu aitwaye yakobo akigombania thawabu/baraka usiku kucha
Mwanzo 32:24-28
24″ Yakobo akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri.
25 Naye alipoona ya kuwa hamshindi, alimgusa panapo uvungu wa paja lake; ukateguka uvungu wa paja la Yakobo alipokuwa akishindana naye.
26 Akasema, Niache, niende, maana kunapambazuka. Akasema, Sikuachi, usiponibariki.
27 Akamwuliza, Jina lako n’nani? Akasema, Yakobo.
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.”
Endapo umeokoka, na unaota upo Katika mapambano kwa kitambo kirefu Hadi unachoka,vBasi ni Mungu anakuasa kwa habari ya Yakobo kwamba tunapaswa utafute sana thawabu zake kuliko kitu kingine chochote katika Dunia hii
2. ISHARA YA VITA
Kuna wakati vita SI Kwa ajili ya kugombania vitu vya thamani Bali wakati mwingine shetani huleta vita tu ili akuangamize.
Wakati mwingine vita huja Kwa ajili ya fitina, kiburi, uadui, chuki n.k
Hivyo basi, unapoota unapigana kwa namna yoyote aidha na mtu, basi hiyo ni vita kutoka upande wa ibilisi ambapo atatumia mapepo, wachawi, majini, au hata watu wa kawaida n.k, hivyo ni vita vya kiroho dhahiri kabisa! Unapaswa uvishinde kwa kuwa karibu na Mungu wako kwa Maombi, sala na kujifunza neno.
Soma..
Waamuzi 9:33
“kisha itakuwa, asubuhi, mara litakapokucha jua, wewe utaamka asubuhi na mapema, na kuushambulia mji huo; tena, angalia, hapo yeye na wale watu walio pamoja naye WATAKAPOKUTOKEA NJE KUPIGANA NAWE, ndipo utapata kuwatenda kama utakavyopata nafasi.”
Ikiwa bado hujaokoka, na unapata ndoto hizi basi chukua tahadhari zifuatazo
• Mpe Yesu Kristo maisha yako, bila kujali dhehebu au dini yako Yesu anaokoa watu wote( Wokovu ni kwa watu wote)
Ukitubu dhambi zako kwa uaminifu na kuziacha Yesu atakuja ndani yako na kukupa roho wake mtakatifu naye atakaa ndani yako milele. Naye atakuongoza katika kumshinda shetani na njia zake zote, Maana wewe upo chini ya kristo Yesu.
Ikiwa upo tayari kufanya hivo fungua somo Hili kuongozwa sala ya Toba na Maombezi
Ndugu mpendwa kumbuka ni siku za Mwisho, na shetani anafanya kazi kwa bidii maana ana muda mchache sana, hivyo Neema ya wokovu iliyofunuliwa kwa watu wote SI ya kupuuziwa!
Fanya maamuzi sahihi na Mungu atakubariki sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.