Maana ya Luka 14:26 “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii Baba yake,

Maswali ya Biblia No Comments

Karibu tuyatafakari Maneno ya Mungu..

Luka 14:26
” Kama mtu akija kwangu naye HAMCHUKII baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Bwana alipoyazungumza Maneno hayo,hakuwa na maana kumdharau au kuwa na uadui, hapana, bali alimaanisha yule apendaye mapenzi ya wazazi au Mtu fulani kuliko mapenzi ya Mungu, huyo hafai kuwa mwanafunzi wake, kwasababu hiyo Bwana wetu Yesu Kristo hawezi kufundisha upendo upande mmoja na mwingine faraka/chuki

Leo ni mkristo anafahamu kabisa kwamba kulewa na kufanya mila za matambiko ni machukizo mbele za Mungu sawa na Neno la Mungu linalopatikana hapa..

Kumbukumbu 18:10 “Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri,

11 wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

12 Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa Bwana; kisha ni kwa sababu ya hayo Bwana, Mungu wako, anawafukuza mbele yako.

13 Uwe mkamilifu kwa Bwana, Mungu wako..

Kwasababu amepata shinikizo kutoka kwa ndugu yake au mzazi wake anashurutishwa na kwa kuwa hana nguvu za rohoni hivyo anakubali ili kuogopa kutengwa na ukoo
Maandiko yanasema mtu huyu hawezi kuwa mwanafunzi wake Yesu Kristo.

Pia bwana anasema mtu asiyezaliwa kwa maji na kwa roho hatauona ufalme Mbinguni lakini kwa kufata dini ya wazazi anaamua kubaki hivyo ingali anajua ya kwamba yapaswa iwe kwa maji mengi na kwa JINA LA YESU KRISTO na ndio ubatizo ambao Bwana anauhitaji, anaacha ibaki hivyo tu, kwa kuogopa ndugu zake au wazazi wake, mtu huyu hawezi kuwa mwanafunzi wake Kristo

kwa maagizo yote tuliyopewa na Bwana hatupaswi kutazama wanadamu wanatoa maoni gani juu ya Hilo, Neno litokapo kwa Bwana tunatii bila hata kusikiliza watu wanasemaje…

Ili ufanyike kuwa mwanafunzi kweli wa Yesu Kristo, huna budi kuingia gharama zake, ni Neema ya Mungu inayotusaidia..

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *