“Kuongozwa sala ya toba”

Maombi na sala No Comments

Unapokuwa tayari kwa hiyari yako kumkabidhi Kristo maisha yako ili akuokoe na kukusamehe dhambi zako basi huo ni uamuzi mzuri zaidi na wenye furaha zaidi maisha yako yote, kama ilivyokuwa kwa sisi wenzako katika kristo Yesu, ilikuwa hivyo hivyo.

Kumbuka..

• kwa Yesu kuna Uzima wa milele, utulivu wa Nafsi na faraja kuu. Kama anavyosema katika

Mathayo 11:28-30
28 “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;

30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

• Kwa Yesu zipo baraka na Msamaha wa kweli

Isaya 1:18
” Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.”

Hivyo ukija kwa Yesu Leo mizigo yako ya dhambi bila kujalisha idadi, haijalishi umezini, umeiba, umekuwa mwasherati ama shetani amekutesa sana kwenye masturbation n.k haitojalisha hayo yote. Bwana Yesu ni Mwingi wa Rehema Wala SI mwingi wa hasira! Unachopaswa kufanya ni kumkiri kwa kinywa chako maana Maandiko yanasema

Warumi 10:9-10
9 “Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.

10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.”

Na..

Warumi 10:13
” kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.”

{Wokovu ni kwa wote!}

Chukua muda mfupi peke yako, tafuta utulivu piga goti ukiwa na utayari kutoka moyoni mwako na ukiri Sala hii kwa Imani, ukijua Bwana yupo pembeni yako akikusikiliza. Sasa SEMA sala hii kwa sauti

EE MUNGU BABA, NAJA MBELE ZAKO, NIKIWA NINAJITAMBUA KUWA MIMI NI MKOSAJI NA NIMEKUTENDA DHAMBI NYINGI, NA KWAMBA NIMESTAHILI HUKUMU. LAKINI WEWE MUNGU WANGU ULISEMA KATIKA NENO LAKO KUWA WEWE NI MUNGU WA REHEMA UNAYEWAREHEMU MAELFU ELFU YA WATU WANAOKUPENDA WEWE. NA LEO HII NINAKUJA MBELE ZAKO NAHITAJI MSAMAHA WAKO NA MSAADA WAKO MUNGU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE KWA KUMAANISHA NA KWA MOYO WANGU WOTE, NINAKIRI KUWA YESU KRISTO NI BWANA, NA YEYE NDIYE MWOKOZI WA HUU ULIMWENGUNI. HIVYO NAOMBA DAMU YA MWANAO TAKATIFU INISAFISHE UOVU WANGU WOTE SASA NIFANYIKE KUWA KIUMBE KIPYA KUANZIA LEO NA HATA MILELE.

ASANTE BWANA YESU KWA KUNIPOKEA NA KUNISAMEHE.

AMEN.

Sasa basi ikiwa umefuatisha maneno hayo kwa Imani basi Umeokoka! Kilichobaki ni kujithibitisha Toba yako kwa vitendo.
Yaani kuyaacha maisha yako ya dhambi uliyoyaishi kabla ya wokovu, Mungu anapoona geuko lako la dhati moyoni mwako, Basi ataipokea Toba yako na kuja kwako kufanya makao ya milele.

Vilevile utafute kanisa la kiroho jirani yako ili umwabudu Mungu wako, na kujifunza Biblia kwa kusudi la kuukulia wokovu wako, na upate ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa Jina la Yesu Kristo upate ondoleo la dhambi zako na kutimiza HAKI yote.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *