Elewa tafsiri ya ndoto KUOTA UMEGANDA

Ndoto No Comments

Nakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo

Kwanza kabisa  mara nyingi ndoto kama  hizi wakati mwingine huwa zinakuja kwa  namna  ya kupambana na Hali fulani ukitumia jina la Yesu Ambapo mwanzoni huwa na upinzani Fulani lakini baadaye inaachia yenyewe kadri uzidivyo kuomba Basi mpendwa huo ni ujumbe kutoka kwa Mungu

Mfano, Mtu anaota anapambana na wachawi na mwanzoni wale wachawi wanakuwa wanamshinda, lakini kadri anavyokemea Kwa jina la Yesu anawashinda, Wengine huota wamekutana na mapepo, punde wakikemea tu sauti hazitoki! Lakini kadri wanavyokazana kuliita jina la Yesu wanawashinda.
Wengine pia hiyo huja kama Hali fulani ya udhaifu, Ambao nao huleta upinzani mkubwa mwanzoni lakini mwishowe hushinda katika jina la Yesu

Angalia, hizo zote ni jumbe za aina moja, ambapo ni Mungu anakuonesha silaha pekee iwezayo kukupa ushindi dhidi ya Shetani ni Jina la Yesu

Hivyo imekupasa kuwa na bidii ili kupata mamlaka kamili juu ya Hilo.
{Mamlaka hiyo huja kwa kulielewa vizuri neno lake na hapo Ndipo kuwepo na nguvu juu ya kutamka kwako} Yaani kumjua zaidi Yesu Kristo.

Tusome..

Yohana 15:7
“Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

Sababu nyingineyo ya kuijua kuhusu ndoto za aina hii, na kwa wengine huja kiuhalisia kabisa kitandani yaani mtu anatamani anatamani ata kuomba asaidiwe kusogeza japo mkono lakini hawezi kuongea, Wengine huenda wakaona kwamba mtu huyo amekufa lakini yeye anajiona bado yupo hai.
Hapo ndugu Unaoneshwa uhalisia halisi wa jinsi mtu anavyokufa, hivyo kazi yako ni kutafakari maisha yako baada ya kifo. Wengine hujidaganya Wakisema ukifa unakuwa hujui chochote, La! Ukifa roho yako inatolewa katika mwili ili nakupelekwa sehemu nyingine(roho haifi) muhubiri 12…

Mpendwa siku ya kufa Kila mtu ataona jinsi anavyoacha mwili wake na kuwaacha wale waliomzunguka,
Sasa ni JE tumejiandaaje na safari yetu hii kwa jinsi tunavyoishi Kila mmoja kwa Nafsi yake.

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *