ELEWA TAFSIRI YA NENO BISI (Ruthu 2:14)

Maswali ya Biblia No Comments

Jina la Bwana Yesu kristo Lihimidiwe.

SWALI: JE! _Bisi ni Nini kama ilivyotumika katika kitabu Cha Ruthu 2:14 na Walawi 23:14_

JIBU: Bisi ni kama tunavyofahamu kwa mazingira yetu kwamba ni yale Mahindi yanayokaangwa na kufutuka, na kuwa na mwonekano mwingine wenye weupe weupe hatimaye kuliwa.

Maarufu zaidi kwa jina la kigeni “popcorn”

Lakini kwa Wayahudi na watu wa Jamii za mashariki ya kati bisi zao si za mahindi Bali ngano lakini hatua za maandalizi ni zilezile kama za bisi za mahindi utofauti unaonekana katika mwonekano wake na rangi Ambayo ni njano.

Hivyo tunapokutana na neno bisi katika biblia basi hizi za ngano ndizo hulengwa sio zile za Mahindi

Mfano, Katika Maandiko Mungu anawapa maagizo Wana wa Israeli pindi watakapovuna mazao yao ya kwanza, Wasile chochote kati ya mavuno hayo si bisi, Wala masuke, mpaka pale watapotoa kile kinachostahili Kwa Mungu

Tusome

Mambo ya Walawi 23:14

” Nanyi msile mkate, wala bisi, wala masuke machanga, hata siku iyo hiyo, hata mtakapokuwa mmekwisha kuleta sadaka ya Mungu wenu; hii ni amri ya milele katika vizazi vyenu katika makao yenu yote.”_

Utakutana nalo katika vifungu hivi

Ruthu 2:14

” Tena wakati wa chakula huyo Boazi akamwambia, Karibu kwetu, ule katika mkate wetu, na ulichovye tonge lako katika siki yetu. Basi akaketi pamoja na wavunaji, nao wakampitishia bisi, naye akala akashiba, hata akasaza.”

 1 Samweli 17:17-18

[17] “Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa uwachukulie ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako;

[18] ukampelekee akida wa elfu yao jibini hizi kumi, ukawaangalie, wa hali gani, kisha uniletee jawabu yao.”

 1 Samweli 25:18-19

[18]” Ndipo Abigaili akafanya haraka, akatwaa mikate mia mbili, na viriba viwili vya divai, na kondoo watano waliofanyizwa tayari, na vipimo vitano vya bisi, na vishada mia vya zabibu, na mikate ya tini mia mbili; akavipakia vitu hivi juu ya punda.

[19] Akawaambia vijana wake, Haya! Tangulieni mbele yangu; angalieni, mimi nawafuata. Ila hakumwambia mumewe, Nabali.”

 

Yoshua 5:10-11 

[10]” Basi wana wa Israeli wakapanga hema zao huko Gilgali; nao wakala sikukuu ya pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi, jioni, katika nchi tambarare za Yeriko.

[11 ]Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo.”

Pia utaikuta katika 2 Samweli 17:28

Tunapaswa kujifunza Nini Tunaposoma Andiko hili?

Nasi tunakumbushwa kutenga FUNGU linalomastahili Mungu kwanza, kwa Kila tunachobarikiwa iwe ni mazao au fedha kabla ya kufikiria Matumizi yetu wenyewe yaani kula n.k

Mungu anatumia bisi kutoa Agizo Hilo kwasababu ni chakula kilicho chepesi zaidi kukiandaa ni kitendo Cha kubandika sufuria na kuepua na Kisha kuitwaa ngano hiyo na kuila tofauti na vyakula vingine vinavyohitaji Maandalizi marefu kidogo.

Hivyo basi hata sisi tunapobarikiwa chochote na Mungu tusikumbuke jambo lolote hata jepesi kama vocha, nauli, manunuzi ya nyumbani n.k kabla ya yote basi  tujatenga FUNGU la Mungu wetu pembeni.

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *