FAHAMU MAANA YA KIMIAMI (Wimbo ulio Bora 2:9)

  Maswali ya Biblia

Jina la YESU kristo Lihimidiwe. Karibu tujifunze Biblia

Wimbo Ulio Bora 2:9
“Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani.”

Kwanza kabisa KIMIAMI ni dirisha kubwa lililo katika GHOROFA.
Hivyo Madirisha makubwa yaliyo katika ghorofa (sio yaliyo katika nyumba za chini)ndiyo hayo huitwa kimiami.

Mfano ni lile dirisha ambalo mfalme ahazia alianguka na kuugua

2 Wafalme 1:2
” Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu.”

Na pia lile ambalo matowashi walimwangusha YEZEBELI
2 Wafalme 9:30-33

30″ Hata Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia uwanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani.

31 Hata Yehu alipoingia lango la mji, alisema, Je! Ni amani, Ewe Zimri, mwenye kumwua bwana wako?

32 AKAINUA USO WAKE KUKIELEKEA DIRISHA, akasema, Aliye upande wangu ni nani? Matowashi wawili watatu wakachungulia.

33 Akasema, Mtupeni chini. Basi wakamtupa chini; na damu yake ikamwagika nyingine juu ya ukuta, na nyingine juu ya farasi, naye akamkanyaga-kanyaga.”

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT