FAHAMU MAANA YA “ULIMI LAINI HUVUNJA MIFUPA” (Mithali 25:15)

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana yesu kristo Asifiwe. Karibu Tuyatafakari Maandiko 

Nini maana ya mstari huu “Na ulimi laini huvunja mifupa “(Mithali 25: 15 )

Mithali 25:15

” Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.”

JIBU: Ukweli ni kwamba ulimi ndiyo kiungo laini zaidi katika mwili, lakini Biblia inatufunulia kwamba kina uwezo mkubwa.

Naam, hata kuvunja Mifupa.

_JE! Kinavunjaje Mifupa?_

Kuvunja Mifupa hiyo ni lugha ya kimithali tu, inayomaanisha kina uwezo wa kuleta athari au matokeo makubwa zaidi ya vile kinavyodhaniwa.

1. Ulimi unapotumika vyema huleta Suluhu ya matatizo makubwa yaliyoshindikana..

2. Vilevile usipotumika vyema, huweza kuleta matatizo makubwa kupita kiasi. 

Turejee katika Maandiko pale ulimi ulipotumika Vibaya na kuleta Matatizo

Kwa sababu tu ya kutumia ulimi pasipo na Busara, Mtoto wa Suleman anasababisha taifa la Israel kugawanyika mara mbili.

Na alilisema Hilo kutokana na malalamiko ya baadhi ya wayahudi kuomba wapunguziwe utumwa waliosababishiwa na babaye Suleman. Lakini tunaona mtoto wa Suleman anatumia mashauri ya vijana wenzake badala ya Yale ya Wazee, Na hivyo badala ya kuwapooza wananchi kwa maneno Mazuri yenye Busara, akawaambia atazidisha Utumwa maradufu ya vile alivofanya Baba yake.

Maneno hayo yaliwakasirisha sana Wayahudi wengi kiasi Cha kukataa kutawaliwa na Uzao wa daudi Tena na hatimae kujitenga. Hapo ndio ikawa chanzo Cha kugawanyika mataifa mawili ndani ya nchi moja ( yaani Israel na yuda) kwa miaka mingi sana.

Mfano mwingine katika Maandiko Ulimi ulipotumika Vibaya

1 Wafalme 12:13-16

13 “Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa;

14 akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge.

15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Bwana, ili alitimize neno lake, Bwana alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.

16 Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.”

Mfano katika Maandiko ambapo ulimi ulitumika vizuri na kubatilisha Mashauri Mabaya

Ni pale Mfalme Daudi alipoonesha Wema wake kwa MTU aliyeitwa Nabali, Pamoja na hayo Pale naye alipotaka Chakula, Nabali alimjibu majibu ya kashfa na kughadhibisha, hivyo Daudi akaapa kwenda kuangamiza nyumba nzima ya Nabali japo aliisaidia hapo kabla. Lakini alipokuwa njiani mkewe Nabali anapata taarifa kuwa Daudi na Jeshi lake wanakuja kuangamiza nyumba yao, Ndipo alipomwendea Daudi kwa unyenyekevu, na kwa maneno Mazuri ya Busara na kutuliza ghadhabu ya Daudi, Naam ndipo Daudi anabatilisha mawazo yake mabaya ya kuangamiza Nyumba hiyo

Tusome

 1 Samweli 25:21-31

21 Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu cho chote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.

22 Mungu naye awafanyie hivyo adui za Daudi, na kuzidi, nikimwachia katika wote walio wake hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi.

23 Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifulifuli, akainama mpaka nchi.

24 Akamwangukia miguuni pake, akasema, Juu yangu, bwana wangu, juu yangu mimi na uwe uovu; tafadhali mjakazi wako na anene masikioni mwako, nawe uyasikilize maneno ya mjakazi wako.

25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.

26 Basi sasa, bwana wangu, aishivyo Bwana, na iishivyo nafsi yako, kwa kuwa Bwana amekuzuia usimwage damu, tena usijilipize kisasi mkono wako mwenyewe, basi sasa adui zako, na hao wamtakiao bwana wangu mabaya, wawe kama Nabali.

27 Na sasa zawadi hii, mjakazi wako aliyomletea bwana wangu, na wapewe vijana wamfuatao bwana wangu.

28 Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika Bwana atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya Bwana; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.

29 Na hata ijapokuwa binadamu angeinuka akuwinde, na kuitafuta nafsi yako, hiyo nafsi ya bwana wangu itafungwa katika furushi ya uhai pamoja na Bwana, Mungu wako; na nafsi za adui zako ndizo atakazozitupa nje, kama kutoka kati ya teo.

30 Tena itakuwa, hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu sawasawa na mema yote aliyoyanena juu yako, na kukutawaza juu ya Israeli;

31 hili halitakuwa kwazo, wala chukizo la moyoni kwa bwana wangu, ama ya kuwa umemwaga damu bure, ama ya kuwa bwana wangu amejilipiza kisasi mwenyewe; tena hapo Bwana atakapokuwa amemtendea bwana wangu mema, ndipo umkumbuke mjakazi wako.”

Na biblia inahitimisha kwa kusema

 Yakobo 3:5-9

5″ Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.

6 Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi, huuwasha moto mfulizo wa maumbile, nao huwashwa moto na jehanum.

7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.

8 Bali ulimi hakuna awezaye kuufuga; ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

9 Kwa huo twamhimidi Mungu Baba yetu, na kwa huo twawalaani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa Mungu.”

Hivyo Wapendwa tujiadhari sana na matumizi ya Ndimi zetu. Maana kwa hizo tutajuangamiza wenyewe na kwa hizo ndipo tunapojibariki Wenyewe.

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *