fahamu maana ya Isaya 59:5 Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui

  Maswali ya Biblia

Isaya 59:5
[5]Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.

Mstari huu humaanisha asili ya watu wabaya.

Anasema huangua mayai ya fira. Fira Kwa Kiswahili kingine ni swila au Kwa lugha inayo tambulika na wengi ni kobra ni aina ya jamii ya nyoka wenywe sumu Kali sana Kwa kawaida mtu akikutana nao lazima amuue au hata kumkimbia na akiona mayai yao lazima ata yahalibu kwasababu asipo Fanya hivyo yaki anguliwa vita leta madhara lakini mtu mwovu kwenye neno la Mungu linasema kinyume chake yeye ata ya angua.
Ikiwa ina maana ya kwamba mtu atakapo ona mabaya yanakuja Kwa watu wengine yeye ata yadhuia ila ata yaacha yaje

Mfano wa hawa watu ni manabii wa uongo wao wanajua fika kuwa bila ya utakatifu hakuna atakaye enda mbinguni(waebrania 12:14)

hivyo kwasababu hawataki kupoteza watu Kwaajili ya tamaa ya fedha hawakemei watu dhambi zao ila badala yake ndo huwa sogeza kwenye Mambo ya mwilini tu juu ya mali,biashara na mambo mengine kama hayo na mwisho wake wana sahau kuhusu Mungu na wana starehe kwenye dhambi zao na wanapo kufa hujikuta wapo kuzimu.

Na vile vile anasema na kusuka wavu wa buibui. Ni kama tunavyo tambua na kuelewa buibui huwuka wavu wake Kwa ajili ya kunasia wadudu ale.

Hivyo hivyo asili ya watu wabaya ndiyo ilivyo huandaa kila namna ya wenzao kunaswa katika mambo maovu na kuangamia.

Mfano unapo mwombea adui yako apatwe na mabaya au afe hapo ni sawsawa ume suka wavu wa uhalibifu. Bwana wetu yesu alisema waombee ila sisi tuna watakia maovu na mabaya hata wafe kabisa tena Kwa maombi.

Hivyo tabia hii ya kutengeneza na kama sio kufurahia anguko la wengine.

Hivyo biblia inatuambia pia tukiwa na tabia kama hizo, zinatufanya na sisi Mungu asitujibu na kutupa haki zetu kwa vile tumwombavyo, nasi majibu yanakuja kinyume chake.. Pale tunapotazamia jema linakuja baya,na  tunapotazamia nuru linakuja giza, tunalithitibitisha hilo katika vifungu vinavyofuata..

Isaya 59:6-9

6 Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.

7 Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao.

8 Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.

9 KWA SABABU HIYO HUKUMU YA HAKI I MBALI NASI, WALA HAKI HAITUFIKILII; TWATAZAMIA NURU, NA KUMBE! LATOKEA GIZA; TWATAZAMIA MWANGA, LAKINI TWAENDA KATIKA GIZA KUU

Hivyo tuombe kwa bidii zote tusiwe vyombo vya shetani vya kuunda mabaya kwa watu wengine. Maana mwisho tutalipwa kipimo kile kile tuwapimiacho wengine inawezekana kutokuwa combo cha shetani kataa kabisa kutoka ndani yako na Yesu Kristo yupo kukusaidia.!

Maranatha!.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT