NI KWA NAMNA GANI NCHI ILIGAWANYIKA (MWANZO 10:25)

  Maswali ya Biblia

Swali:Je ni kweli nchi au dunia iligawanyika? Je iligawanyika kwa namna gani? Je haya mabara saba yaliyopo yalitokana na huo mgawanyiko?

JIBU

Mwanzo 10:25 “ Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza ni Pelegi maana KATIKA SIKU ZAKE NCHI ILIGAWANYIKA; na jina la nduguye ni Yoktani”.


Ukisoma zaidi sura ya 11 katika kitabu hicho cha Mwanzo utaona habari za kujengwa kwa mnara wa babeli.. Wakati ule watu walikuwa wameanza kuujenga mnara wa babeli na ndipo Mungu alishuka na kuchafua usemi wao ili wasiweze kusikilizana na ndipo waliposambaa kila mtu na njia yake.

Mwanzo 11:1-4,6-9
[1]Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.


[2]Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.


[3]Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.


[4]Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.


[6]BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.


[7]Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.


[8]Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.


[9]Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.


Mstari wa 8 unasema ‘BWANA AKAWATAWANYA KUTOKA HUKO WAENDE USONI PA NCHI YOTE’

Kutawanyika kwa watu maana yake ni kugawanyika kwa nchi ambako tunasoma katika Mwanzo 10:25 na tunaona mgawanyiko unajirudia tena katika kitabu cha 1Nyakati 1:19, tunaona hapo ulitokea wakati ambao Pelegi mwana wa Eberi aliishi.

Hivyo maandiko hayasemi kuwa mabara saba yalitokea hapo, hapana ila tunona mgawanyiko wa watu yawezekana haya mabara saba yalikuwepo tangu dunia inaumbwa,au yalitokea kipindi fulani baada ya uumbaji ambacho hakijatajwa katika kitabu cha Mwanzo 10:25. Kwa hiyo tunaona watu ndio waligawanyika na sio mabara..


Shalom

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT