Neno Sharoni maana yake ni “uwanda” au “nchi tambarare”. Katika maandiko tunaona kuna eneo(wilaya) ambalo linajulikana na kufahamika sana na waisraeli kama sharoni ijapokuwa katika biblia hakuna maelezo mengi yaliyotolea kuhusu eneo hilo. Ingawa ni eneo ambalo lilikuwa na rutuba nyingi, na pia lipo karibu sana na fukwe za bahari kubwa ya Mediterenia , waweza thibitisha katika ramani. japokuwa biblia haijatolea maelezo yake mengi, Lakini ni eneo lililokuwa na rubuta nyingi, na lilikuwa lipo karibu na fukwe za ile bahari kubwa(yaani bahari ya Mediterenia)
Utasoma Neno hilo kwenye vifungu hivi vya biblia;
Nyakati 5:16 “Nao wakakaa huko Gileadi, katika Bashani, na katika miji yake, na katika viunga vyote vya Sharoni, hata kufika mipakani mwake”.
1Nyakati 27:29 “na juu ya makundi ya ng’ombe waliolishwa katika Sharoni alikuwa Shitrai, Msharoni; na juu ya makundi waliokuwamo mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai”;
Isaya 33:9 “Nchi inaomboleza, na kulegea; Lebanoni imetahayarika na kunyauka; Sharoni imekuwa kama jangwa; Bashani na Karmeli zimepukutika majani”.
Isaya 65:10 “Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta”.
Na katika agano jipya utalisoma katika kifungu hichi;
Matendo 9:35 “Na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana”.
Pia tukisoma katika kitabu cha wimbo ulio bora, tunaona katika maandiko kuwa lipo UA moja ambalo maandiko yanalitaja kama UA la Uwandani au kwa jina lingine ni UA la sharoni. Vivyo hivyo Mwandishi wa kitabu cha wimbo ulio bora na yeye anajifananisha kama Ua hilo ambalo limechipuka katika nchi hiyo ya Sharon
Wimbo 2:1 “Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni.
2 Kama nyinyoro kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti”.
Bila shaka Ua hili ni Yesu kristo mwenyewe na ndiyo yeye ndiye aliechipuka katika bonde la ulimwengu yaani kuja kwake Bwana wetu Yesu kristo ulimwenguni na alikuwa na mwonekano tofauti na wanadamu wengine.
Ndiye aliekuja kubeba mzigo wa maovu/ dhambi yetu kwa kutufilia pale msalabani. Nakupelekea kupata kibali mbele za Mungu yaani kurejesha Mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu tena. Maana yeye ndio Bwana na mwokozi wa ulimwengu huu …
Je! Na wewe umapata kuoliona Ua hilo?, Je umempata nafasi ya kumpokea mwokozi ndani ya moyo wako?
Kumbuka hakuna namna nyingine ya kumfikia Mungu isipokuwa kwa kumpokea na kumkiri Bwana Yesu yakuwa ndie Bwana na Mwokozi wa maisha yako … Uamuzi ni wako ? nyingine yoyote utakayoweza kumfikia Mungu isipokuwa kwa njia yake yeye. Hakuna mwanadamu yoyote anayeweza kumpendeza Mungu kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa Yesu Kristo peke yake. Ukimkosa Kristo maishani mwako, haijalishi umepata ulimwengu mzima, hesabu kuwa umepoteza kila kitu.
Lakini ukimpokea yeye, hata ukikosa vyote hesabu kuwa umevipata vyote, uamuzi ni wako, kumbuka hizi ni siku za mwisho, Lakini ikiwa leo utapenda kuyakabidhi maisha yako kwake, Huo utakuwa ni uamuzi wa busara sana,
Shalom.
Bwana akubariki
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.