JE  ADAMU NA HAWA WALIKWENDA MBINGUNI BAADA YA KUFA?

Maswali ya Biblia No Comments

JIBU..

Maandiko hayajatupa uwazi wa moja kwa moja wa kuelewa kama waliokoka au hawakuokoka pindi walipofahamu uovu walioufanya.. Tukiliangalia hili neno Kuokoka tunakuja kuliona kwenye kipindi chetu cha Agano jipya likiwa na maana ya kukombolewa kwenye uharibifu wa hukumu ya Mungu iliyoikumbuka ulimwengu mzima kwasababu ya dhambi kupitia kifo cha Mwokozi Yesu Kristo anayetuokoa sisi na hukumu hiyo..

Hivyo tunaweza kupata ufahamu watu wa Agano la kale pia walipata kuokolewa kwa kutii ile ahadi ya Mungu aliyoiahidi ya kumleta masihi duniani baadae,ambaye ni Yesu Kristo..Kiuhalisia waliokwenda na imani hiyo kwa Mungu walipata kuokoka kwa kuwa ahadi ya Mungu ilimkusudia kweli Mwokozi Yesu Kristo..

Tukiyaangalia baadhi ya matukio yaliotokea kipindi cha Agano la kale yote yanamuakisi Yesu Kristo,

Mfano wa ile safina aliyoitengeneza Nuhu,ni Yesu Kristo, Ule mwamba ambao wana wa Israeli waliposikia kiu,maji yakatoka,sasa ule Mwamba ni Yesu Kristo,kwa kuwa wote walioukataa fahamu walimkataa Yesu (1Wakorintho 10:4), tukiangalia tena yule nyoka wa shaba jangwani, walioumwa nae na kukataa kuitazama hiyo nyoka,basi walimkataa Yesu Kristo (Yohana 3:14) pamoja na zile amri mbili walizopewa na Musa waliokataa kuzitii walimkataa Kristo, yule melkizedeki aliyekuja kwa Ibrahim alikuwa Yesu Kristo, wale malaika waliokwenda sodoma alikuwa ni Kristo ndani yao..

Hivyo tunaona kila mahali ni Kristo alijidhihirisha kwao kwa picha ya maumbo na vivuli kusudi ni ili wamwamini yeye, na wote waliomwamini waliekwa kwenye kundi la watu ambao siku Kristo atakapofunuliwa basi nao watakuwa kwenye usalama wa kuokolewa, na ndo mana unaona hata siku Yesu anafufuka biblia inasema miili mingi ya watakatifu ikafufuka na kutoka makaburini na kupelekwa peponi, kwenye raha ya Yesu mwenyewe, kwasababu hapo kabla watakatifu waliokufa walikaa tu kwenye makaburini Lakini tokea kufufuka kwa Bwana Yesu wanapelekwa peponi..

Kwa msingi huo utatupa kuelewa kama Adam na hawa walimtii Kristo au sivyo” lakini biblia inatuonyesha baada ya adamu na mkewe kujiona wako uchi hawana nguo hawakuendelea kufurahia hali hiyo, hapana, bali walipojiona wapo uchi walijificha ikionyesha walijutia dhambi waliyoitenda na ndo hapo tunaona Mungu anamchinja mnyama na kuwapa ngozi wajifunike lakini sisi ndo tunaofahamu huyo mnyama alimfunua Kristo (Mwanzo 3:21) na kama wangekataa basi wasingeweza kuokoka,…

Na ndo maana Bwana anatuambia sisi wa siku hizi za mwisho Kuhusiana na kuvikwa vazi ili aibu yetu iondoke..

Ufunuo 3:18  Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na MAVAZI MEUPE UPATE KUVAA, AIBU YA UCHI WAKO ISIONEKANE, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona

Biblia inatuonyesha pia kuwa uzao wa mwanamke ndio utaoponda kichwa uzao wa nyoka, ikionyesha kuwa hawa hakuwa na ushirika na uzao wa adui (Mwanzo 3:15)

Na Watoto wao pia tunaona wakina sethi walikuwa wakimtolea Mungu sadaka zao na matoleo ambayo yalimfunua Kristo Katika umbo, wasingeweza kutenda au kufanya mambo hayo kama wasingeyaona na kuyafahama kutoka kwa wazazi wao…

Sababu nyingine tunaona Kristo anafahamika kama ,Mwana wa Adamu, tunaona hata ule uzao uliorodheshwa anatajwa kama “wa Adamu(Luka 3:23-38) na asingeitwa kwa jina hilo la Adamu kama angekuwa ni uzao wa ibilisi,Mungu hawezi kujichanganya, ni yeye yule yule,ni mshindi milele yote,mwanzo na mwisho atabaki kuwa Mshindi..

Hivyo kwa hitimisho ni kuwa Adamu na hawa hawakupotea bali walimwamini Yesu Kristo baada ya kuanguka Katika dhambi na waliokoka…

Ubarikiwe..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *