Je? Kuna watu walioumbwa kabla ya Adamu?

  Maswali ya Biblia

Shalom Karibu tuyatafakari maandiko kwa pamoja.

SWALI : JE! Kuna watu wengine Mungu aliwaumba kabla ya Adamu? Katika

Mwanzo 27:1 Tunaona Mungu aliumba Mwanamke na mwanaume, Tena katika Mwanzo 2:7 tunaona anaumba mtu mwingine yaani Adamu. 

Kitabu Cha Mwanzo sura ya kwanza kinazungumzia Uumbaji wa Mungu kwa Muhtasari yaani kwa ufupi sana, Lakini tunapoendelea kusoma mpaka Ile sura ya pili ndipo Unaelezewa kwa upana/Urefu zaidi.

Hivyo mlango wa kwanza ni muhtasari na ndio Maana mambo yanaelezwa kwa ufupi tu.

Mfano

Mwanzo 1:11-13
11 “Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.

12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.

13 Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya tatu.”

Hapa utaona Uumbaji wa miti na mimea ukielezwa kwa ufupi sana, haijaelezwa ulitokeaje tokeaje, Hivyo tunapotaka undani zaidi wa Uumbaji wa mimea ulitokeaje tokeaje tunaenda mlango wa pili ambako ndipo kuna undani zaidi wa Hilo

Tusome

Mwanzo 2:4-6
4 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

5 hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

6 ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.”

Kama tunavyoona, Kumbe kabla Mungu hajasema nchi itoe majani na mche utoao mbegu, siku Ile Ile aliinyeshea Mvua na ndipo ikazaaa mimea miti n.k
Hii Ina maanisha hakusema tu miti itokee nayo ikatokea kumbe kumbe kulikuwa na mchakato(process) ulioendelea kabla ya hapo, Ambao huo tunakuja kuupata katika mlango wa pili.

Vivo hivyo Mungu aliposema katika

Mwanzo 1:27
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, Mwanaume na mwanamke aliwaumba

Uumbaji wa mwanadamu Unaelezewa kwa ufupi, yaani haijaweka bayana mwanamke na Mwanaume waliumbwaje umbwaje!?, na JE waliumbwa wote kwa pamoja? na kwa malighafi Gani? Vyote ni fumbo katika mlango wa kwanza, na linafumbuliwa kwa uwazi katika mlango wa pili

Tusome..

Mwanzo 2:4-8
[4]”Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi

[5] hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi;

[6] ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

[7] BWANA MUNGU AKAMFANYA MTU KWA MAVUMBI YA ARDHI, AKAMPULIZIA PUANI PUMZI YA UHAI; MTU AKAWA NAFSI HAI.

[8] Bwana Mungu akapanda bustani upande wa mashariki wa Edeni, akamweka ndani yake huyo mtu aliyemfanya.”

Hapo utaona Maandiko yanaweka wazi kwamba Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi jambo ambalo sio bayana katika sura ya kwanza(Mwanzo 1:27)
Unapoendelea zaidi Hadi Mwanzo 2:18-24 Imeonesha wazi Hadi jinsi mwanamke alivyoumbwa kwa kutwaliwa kutoka ubavuni mwa Mwanaume, Hili pia halikuwa bayana katika mlango wa Kwanza.

Kwahiyo Uumbaji katika Mwanzo mlango wa kwanza ni muhtasari wa Uumbaji wa Mungu, maelezo zaidi yanapatikana katika mlango wa pili. Ni sawa sawa na Unaposoma kitabu Fulani kunakuwa na Ile ” table of contents/Yaliyomo” Ambayo kuna mkusanyiko wa yote yanayopatikana katika kitabu hicho, mfano huu ni sawa sawa kabisa na hapa katika kitabu Cha Mwanzo sura ya kwanza na sura nyinginezo zaidi yaani ya pili hadi 50.

Kwa kuyaona hayo yote.. SI kweli kwamba kuna mwanadamu aliumbwa kabla ya Adamu na Hawa, Kimaandiko Hawa ndio binadamu wa kwanza kuumbwa!!
Baada ya Uasi walifukuzwa katika bustani ya edeni, na kuanzia hapo wote tunaozaliwa tunalibeba anguko hilo. Mpaka pale tunapozaliwa mara ya pili kwa uzao mpya wa Adam wa pili yaani “Yesu Kristo” ambaye pamoja na kujaribuwa hakutenda dhambi hata mara moja! Na huyo amefanyika kuwa mkombozi wetu.

Maandiko yanasema Kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi naye hataishi tena chini ya laana bali chini ya Baraka.
Lakini wote wasiomwamini hawatapata ondoleo la dhambi badala yake Ile siku ya mwisho watatupwa katika ziwa la moto, aliloandaliwa Shetani na malaika zake.

JE wewe ni miongoni mwa waliomwamini? au wasiomwamini?
Kama bado hujamwamini Yesu tambua dhahiri ya kwamba upo
Chini ya laana ya anguko la Adamu, na hakuna njia nyingine yoyote ya kuhesabiwa haki bali kumpokea yesu maishani mwako, haitajalisha mazuri Mangapi utakayoyafanya maishani mwako hutamwona Mungu. Yeye pekee ndio njia pekee ya kufika Mbinguni hakuna mwingine.

Hivyo mpendwa mpokee Yesu Leo katika maisha yako kwa kutubu dhambi na kudhamiria kuziacha kutoka moyoni. Baada ya Toba hiyo tafuta ubatizo wa kweli kw Jina la YESU kristo ambalo ndilo jina la Baba la mwana na la Roho mtakatifu.
Kwa njia hizo tatu yaani Imani, ubatizo na ujazo wa Roho mtakatifu atakuongoza kuijua kweli yote na ondoleo la dhambi

Shalom.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT