Je umejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii?

Maswali ya Biblia No Comments

Shalom, Karibu tuyatafakari Maneno yenye uzima..

Biblia inasema tumejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, na leo tutajifunza ni msingi gani tunaotakiwa kuufahamu zaidi..

Waefeso 2:20

[20]Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.

Ni kweli kupitia msingi huu wa mitume na manabii ambao ni Mungu mwenyewe aliusimamisha kwa makusudi yake ili tuenende vema Katika safari ya imani,na wengi tunafahamu msingi ambao tunasimama nao mpaka leo ni yale mafunuo ambayo Mungu alikusudia kuyafunua kwa mitume wake na manabii ili kusimamisha kanisa lake..

Ndo mana tunaona hata  Katika agano la kale manabii walitumika kwa asilimia kubwa sana Katika kuwarejeza wana wa Israeli pale walipoingia Katika makosa au walipofanya chochote kilichomkasirisha Mungu, na hapo tunaona Mungu akimtumia nabii fulani na kumpa ufunuo wa Jambo linaloendelea ili akaliweke wazi kwa taifa..

Na sio kila nabii alipewa ufunuo bali yule aliyachaguliwa na Mungu,..

Na sisi wa Agano jipya tumesimamishwa na mafunuo ya mitume kumi na mbili wa Bwana wetu Yesu Kristo, ndio mababa zetu wa imani,ambao walichaguliwa na Bwana kwa makusudi hayo,maana yake hatuwezi kutoka nje ya msingi huo au kusimama ju ya msingi mwingine..

Lakini leo nataka tujifunze msingi mwingine mkuu wa mitume na manabii walioufanya, na msingi huo ni..

KUHUBIRI INJILI

Baada ya kupewa mafunuo makubwa mengine Mpaka ya siku za mwisho hawakuridhika na kuona wameshamaliza kila kitu,walijua wanayo kazi nyingine ya kuufanya msingi wao uwe imara zaidi ni kuwapelekea watu habari hizo njema walizofunuliwa na Mungu, manabii wa kale walihubiri na kwenda mpka nchi za mbali kwa lengo na kuwajulisha mambo ambayo watayapata kama wakikataa kuitii au kuisikiliza sauti ya Mungu iliyofunuliwa kwake,

Ndo hapo tunaaona wengine iliwalazimu mpka kuuwawa, mapigo,kudhihakiwa n.k lakini lengo la kuwahubiria yale Mungu aliyoyakusudia yawe wameyatimiza…

Yeremia 35:15-16

[15]Pia naliwapeleka watumishi wangu wote, manabii, kwenu ninyi, nikiamka mapema na kuwapeleka, nikisema, Rudini sasa, kila mtu na aiache njia yake mbaya, mkatengeneze matendo yenu, wala msiwafuate miungu mingine, ili kuwatumikia, nanyi mtakaa katika nchi hii, niliyowapa ninyi na baba zenu; lakini hamkutega masikio yenu, wala hamkunisikiliza.

[16]Basi, kwa kuwa wana wa Yonadabu, mwana wa Rekabu, wameitimiza amri ya baba yao aliyowaamuru, lakini watu hawa hawakunisikiliza mimi;

Mitume baada ya kukaa na Bwana kwa kipindi chote na kufunuliwa mambo mengi na makubwa, Bwana alijua kazi waliyonayo sasahivi ni yakwenda kuwahubiria watu na kuwafundisha, ndo maana mitume walijitoa kwa hali zote ili kuhakikisha kile walichofunuliwa kinakwenda kuwasaidia na kuwavuta wengine kwa Kristo ,ndo mana siku anaondoka aliwaambia Maneno haya,…

Marko 16:15

[15]Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Akuwaambia nendeni mkapumzike sasa mmeshajua vitu vingi sana,au mkajivune kwa watu kwamba ninyi ni bora, anawaambia mkahubiri hizo habari njema mlizofunuliwa…

Ndugu, ni wengi tunasema tumeokoka tunampenda Yesu, ukimaanisha umesimama juu ya msingi/ ufunuo huu wa mitume ,Jiulize unawahubiria watu hizo habari njema ulizonazo, ikiwa hautoi kwa wengine kile ulichofunuliwa na Mungu fahamu kabisa bado ujasimama vema kwenye msingi huu wa mitume,

Umekuwa kwenye wokovu kwa kipindi kirefu lakini kitendo cha kwenda kuwaambia watu uzuri wa Yesu, Upendo wa Mungu, wewe huna’ bado ujajengwa kwenye msingi, kitendo cha kumwamini Yesu Kristo tayari unasababu nyingi za kuwavuta na wengine wamwamini yeye..

Ukitaka kukamilishwa na kujegwa kwenye msingi wa mitume HUBIRI INJILI..

Warumi 10:15

[15]Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!

Bwana akubariki..

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *