Shalom. Karibu tujifunze maneno ya Uzima
Kumekuwa na udanganyifu mkubwa Leo kwamba ndoto zina tiba! Mpendwa mtu anayekuambia, kama umeota ndoto Fulani basi uende kwake akupe dawa labda umekutana na jini, umefanya uasherati na usiyemjua, umetumbukia shimoni n.k
Huo ni ushirikina na ni Utapeli mkubwa!.
Ndoto au maono hutoka ndani ya mtu hivyo ni mambo ya kiroho hayawezi kutibika kwa Kinga au dawa za NJE kama vidonge au tiba Fulani, mfano huwezi kumganga mtu aliyefiwa na mzazi wake kwa pain killer! Maana maumivu yake yanatoka moyoni na sio nje!
Kwanza kabisa tuanze kuziangalia aina za ndoto
1. Ndoto zinazotokana na Mungu: Huchukua sehemu ya wastani kati zile aotazo mtu Kila siku
2. Ndoto zinazotokana na Shetani: hizi pia Huchukua sehemu ya wastani tu
3. Ndoto zinazotokana na mtu mwenyewe {Shughuli}
Hizi ndizo Huchukua sehemu kubwa zaidi ya ndoto kila siku
Kuota Umetumbukia Shimoni
Au inaweza kuwa upo ukingoni mwa shimo, au tayari upo kwenye shimo refu lenye kiza, au Unaningi’inia katika shimo ukiwa mzito sana, unahitaji msaada wa kuvutwa juu usiwepo. Naamh zote ni jumbe za aina moja.
Sikiliza, utakuwa hatarini sana endapo hutachukua maamuzi sahihi juu ya maisha yako kama Mungu asemavyo na wewe kwa habari hili.
Ikiwa umempa kristo maisha yako {Umeokoka} na umeota ndoto hii mara kadhaa ikiwa na uzito sana, Basi imekupasa kuongeza umakini na Mungu wako maana, kuna mahali utakwama kiimani hata usisonge mbele kiroho.
Ombea sana mazingira uliyopo, kazi unazozifanya Mtangulize Mungu naye atakuvusha asiruhusu uanguke shimoni.
Soma ( yeremia 36:8, Maombolezo 3: 52-57)
Lakini ikiwa wewe hujaokoka na unajihusisha na mambo haya
• Uzinzi
Mithali 22:14
“Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na Bwana atatumbukia ndani yake.”
Mithali 23:27
” Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba.”
Mwisho wa Uzinzi ni mbaya, utaishia kukuingiza mahali usipoweza kutoka milele.
• Kutokutenda HAKI , kumjengea chuki au uhasama mwenzio asiendelee mbele..
Mithali 26:27
” Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia.”
Zaburi 7:14-16
14 “Tazama, huyu ana utungu wa uovu, Amechukua mimba ya madhara, amezaa uongo.15 Amechimba shimo, amelichimba chini sana, Akatumbukia katika handaki aliyoifanya!
16 Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini.”
Yote inajaribu kuelezea madhara ya uovu, kwamba hatma yao Waovu ni shimoni , shimo Hilo ni mauti endapo hatotubu.
Kumbuka ya kwamba Yesu ndiye pekee njia ya kweli na Uzima{ Yohana14:6} hivyo tengeneza na Mungu wako Sasa, Maana anakupenda ndiyo maana anakuita, na anakutaka uache dhambi usafishe maisha yako.
Nani ajuaye huenda huo ni wito wa Mungu wako kwamba “Uokoke Leo”
Hivyo mpe maisha yako Leo, usipuuzie wito huu ili Mungu akuokoe kutoka shimo refu ambalo aidha umeshaingia au upo mbioni kuingia humo.
Ikiwa umekubali kutii na kumgeukia basi Umefanya maamuzi mazuri sana maishani mwako, hivyo ndivyo ilivyokuwa hata kwetu sisi,
Ikiwa umefuatisha sala hiyo, hatua inayofuata ni kujithibitisha kwa vitendo, kwa kudhamiria kuziacha kabisa dhambi zako na kumgeukia Bwana.
Mungu atakapoona hayo basi ataipokea Toba yako na kufanya makao ya milele kwako, vilevile utafute kanisa la kiroho ambalo utamwambudu Mungu, utajifunza biblia na kuukulia wokovu wako, pia upate ubatizo sahihi wa maji mengi na kwa ” Jina la Yesu Kristo” upate ondoleo la dhambi zako.
ubarikiwe sana.
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.