MIIMO ni nguzo mbili za mlango upande wa kulia na wa kushoto wa mlango, kama tunavyosoma katika kisa cha Samsoni akichomoa malango ya Wafilisti.
Unaweza somo vifungu hivi, Kumbukumbu la Torati 6:9, 1 Wafalme 6:33, na Isaya 57:8.
Waamuzi 16:3 “Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, NA MIIMO YAKE MIWILI, akaing’oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni”.
Na
Kizingiti ni nguzo moja ya mlango ambayo iko upande wa juu wa mlango, wakati mwingine huwekwa upande wa chini. mfano pale wana wa Israeli walipotolewa Misri, waliambiwa wapake damu ya mwana kondoo kwenye vizingiti na miimo ili kumzuia Malaika asiingie na kuwaua wazaliwa wa kwanza wa nyumba hizo.
Kutoka 12:7 “Nao watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na KATIKA KIZINGITI cha juu, katika zile nyumba watakazomla”.
miimo na vizingiti vinaweza kutengenezwa kwa malighafi yoyote, kama vile mbao, chuma, udongo, au shaba.
Vitu hivi pia vinadhihirisha jambo la kiroho, miili yetu ni nyumba (hekalu la Roho Mtakatifu) lenye mlango wenye miimo na vizingiti. Mlango wa Hekalu la Roho Mtakatifu ni mioyo yetu, ambayo ina miimo na vizingiti vyake, kama vile macho na masikio yetu. Masikio ni vizingiti, na macho hupokea kile tunachosikia, na macho hupokea kile tunachoona. Ikiwa macho na masikio yetu yatasafishwa kwa damu ya Yesu Kristo, ni sawa na ile nyumba iliyopakwa damu ya mwana kondoo katika miimo ya milango yake na vizingiti vyake nyakati za Israeli kutoka Misri, ambapo ilifanya uharibifu usidhuru nyumba ambazo zilikuwa zimepakwa damu
hivyo nasi hili nyumba zetu ziwe Salama ni lazima Yesu awe ndani yetu maana yeye ndiye mwokozi wa maisha yetu
Ufunuo 3:20 “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”
Basi ikiwa bado ujampokee Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wako ili akuokoe na kukupa nguvu ya kushinda dhambi wakati ni huu
1Wakorintho 3:17 “Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi”.
Basi kama haujampokea Kristo yeye ndiye mlango wa kuingia mbinguni. Yohana 10:7
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.