Nini maana ya masihi?

Maswali ya Biblia No Comments

Masihi ni neno ambalo asili yake ni neno la kiebrania, linalomaanisha MPAKWA MAFUTA.
au Mtu aliyeteuliwa na Mungu Kwa kusudi fulani alijukikana kama masihi.
Katika kipindi cha agano la kale watu ambao Mungu aliwateuwa kuwa wafalme au manabii walijulikana kama Masihi, yaani wapakwa mafuta wa Bwana

Maana nyingine masihi inamaanisha Kristo, kwahiyo basi MPAKWA MAFUTA, au wapakwa mafuta walijulikana pia kama “Makristo”

Lakini japo hawa watiwa mafuta walikuwa wengi ambao waliteuliwa na Mungu katika kulitimiza kusudi la Mungu, lakini Kuna vipindi walikuwa wanakosea
mfano tumsome mtiwa mfuta ambaye alikosea
ambaye hakuwa mkamilifu asilimia zote.

2 Samweli 11

2 Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari ya jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.

3 Naye Daudi akapeleka, akauliza habari za yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, Je! Huyu siye Bath-sheba, binti Eliamu, mkewe Uria, Mhiti?

4 Basi Daudi akapeleka wajumbe, akamtwaa; naye akaingia kwake; naye akalala naye; (maana yule mwanamke amekwisha kutakasika unajisi wake); kisha akarudi nyumbani kwake.

umeona hapo japo daudi alitiwa mafuta, lakini alikosea kwa kitendo cha kumtamani mke wa Uria mhiti, ukiendelea kusoma habari hiyo utaona hadi ilifikia hatua daudi akaamua kumuua kabisa uria.
Na si daudi tu walipokuwepo na wengine ambao japo walikuwa Makristo lakini hawakuwa wakamilifu, mfano sauli
unaweza soma 1 Samweli 24:9

Lakini si kwamba hakukutokea masihi tena aliye kuwa makamilifu, japokuwa wengi kweli hawakuwa wakamilifu asilimia zote, LAKINI ALITOKEA MASIHI AMBAYE ALIKUWA MKAMILIFU ASILIMA ZOTE AMBAYE YEYE HAKUKOSEA TANGU AMETIWA MAFUTA, NAYE SI MWINGINE ZAIDI YA BWANA WETU YESU KRISTO

Waebrania 1:8 “Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

9 Umependa haki, umechukia maasi; Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekutia mafuta, Mafuta ya shangwe kupita wenzio”.

Ndiyo maana hata wasamalia pamoja na waisraeli, walikuwa wakigonja ujio wa masihi ambaye alikuwa mkamifu kuliko hao wengine waliopita, ambaye atakuja kuwatawala na kuleta amani, Kwa sababu ya kukosa masihi ambaye alikuwa mkamilifu ambaye angeweza kuwaongoza

Yohana 1:40 “Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.

41 Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). .

unaweza soma tena

Yohana 4:25 “Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote.

26 Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye”

Lakini ujio wa masihi ambaye ndiye Yesu Kristo, tayari ulishakwisha tukokea miaka elfu mbili iliyopita (2000), japo wayahudi ambao walikuwa wakingojea ujio wake alipokuja walimkataa, na ndio hao hao waliomsurubisha , lakini tunaona jambo hili ndilo lilituletea wokovu, baada ya Yesu kufa alifufuka, akapaa mbinguni kwenda kutuandalia makao ambayo ndani yake hakutakuwa na dhiki wala vita, mgonjwa, njaa na misiba, inajulikana kama ujio wa pili wa Bwana wetu Yesu kristo kuja kukomesha uharibifu wote, na awamu hii hata kuja kama mwokozi tena bali atakuja kutoa hukumu

Je umempa Yesu Kristo maisha yako, je umekubali awe mwokozi wa maisha yako, kumbuka kuwa baada ya kifo ni hukumu ikiwa Leo hii utashindwa kumpokea Yesu Kristo jua kabisa baada ya kufa kwako ni hukumu tu, hivyo mpokee Yesu Kristo Awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako maana hiyo ndiyo salama yako, baada ya hapo batizwa katika ubatizo sahihi ambao ni kwa jina la Yesu sawa sawa na andiko la (matendo 2:38)

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *