BEHEWA NI NINI?

Maswali ya Biblia No Comments

Jibu…

Behewa ni sehemu iliyo wazi ambayo imezungushiwa fensi mbele ya Hema ya kukutania, ilitumiwa na makuhani kama eneo la kutoa sadaka za kuteketezwa na shughuli mbalimbali za kikuhani, unaweza ukatazama picha iliyopo juu, na kwa jina lingine inafahamika kama UA.

Katika kipindi cha Mfalme Suleimani pale Yerusalemu sehemu ya ua/behewa palizingushiwa ukuta, pakawa na ua kuu mbili ya kwanza ya ndani na ya pili ni ya nje, ya ndani ilikuwa maalumu kwaajili ya makuhani tu na ya nje ikawa sehemu ya Wayahudi kukutanika na kufanya ibada, unaweza ukatazama picha iliyopo chini

Katika biblia behewa/ ua haikuwa kwenye Hema ya kukutania pekee bali pia hata kwenye majumba ya kikuhani na kifalme..

1 Wafalme 7:1
[1]Naye Sulemani alikuwa katika kuijenga nyumba yake mwenyewe miaka kumi na mitatu, akaimaliza nyumba yake yote.

12 Na behewa kubwa pande zote ilikuwa na safu tatu za mawe ya kuchongwa, na safu moja ya mihimili ya mierezi; mfano wa behewa ya ndani ya nyumba ya Bwana, na ukumbi wa nyumba”.

Mathayo 16:3 “Wakati ule wakuu wa makuhani, na wazee wa watu, wakakusanyika katika behewa ya Kuhani Mkuu, jina lake Kayafa”;

Kwenye kitabu cha Ufunuo wa Yohana kinatuonyesha kuwa wakati wa mwisho Wayahudi wa Yerusalemu watajenga behewa na litamilikiwa na watu wa mataifa kwa mda wa mitatu na nusu( miezi 42)

Ufunuo 11:1 “Nikapewa mwanzi kama fimbo; na mmoja akaniambia, Inuka, ukalipime hekalu la Mungu, na madhabahu, na hao wasujuduo humo.

2 Na behewa iliyo nje ya hekalu uiache nje wala usiipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arobaini na miwili”.

Ili kupata maana yake rohoni kuhusiana na mambo hayo unaweza kukutafuta kupitia namba hizi. +255 693 036 618/+255 789 001 312

Ubarikiwe.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki..

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *