NINI MAANA YA IKABODI?

Maswali ya Biblia No Comments

Neno IKABODI tafsiri yake ni “Utukufu umeondoka”

Jina hili alipewa mtoto wa Finehasi na mke wake wakati anajifungua, baada ya kupata taarifa mumewe amekufa katika vita, pia sanduku la agano limechukuliwa na wafilisti na yeye mkewe wa Finehasi anakaribia kufa ndipo akampa mtoto huyo jina la IKABODI, akiwa na maana utufuku wa Mungu umeondoka katika Israeli.

1Samweli 4:19 “Tena mkwewe, mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa, akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia.

20 Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini hakujibu, wala hakumtazama.

21 Akamwita mtoto, IKABODI, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.

22 Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa”.

Yote hayo kwasababu ya makosa ya watoto wa Kuhani Eli ambao ni Finehasi na Hofni kwa kuitia unajisi madhabahu ya Mungu, kwa kuzini na wanawake waliokuwa wakihudumu hemani pa Bwana. Na mara nyingi walionywa lakini hawakutaka kusikia, ndipo Bwana kupitia Mtumishi wake Samweli akamwambia Kuhani Eli kuwa nitafanya Jambo ambalo watu wakisikia masikio yao yatawasha. Ndipo likatokea tukio ambalo halikuwahi kutokea katika Israeli la kuchukuliwa kwa Sanduku la Agano na Wafilisti.

Pia katika Kanisa lolote lile utukufu unaweza ukaondoka kwasababu ya watumishi wa Mungu kufanya maovu ambayo wanajua wazi Kabisa hayapendezi mbele za Mungu na huku wanaendelea kuyafanya.

Lakini ata kwa mtu utukufu unaweza ukatokewa kutokana na kufanya yale ambayo si mema machoni pa Bwana ikiwa mtu ameonywa mara kadhaa mfano kuacha uzinzi,ulevi,uongo,kubeti lakini bado anaendelea kuyafanya

Hivyo wakati ni Sasa wa kutubu na kumgeukia Bwana, na ikiwa upo nje ya Kristo mda ni Sasa wa kutubu na kubatizwa katika Ubatizo sahihi

Ubarikiwe

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *