Nini Maana ya Korbani?.

Uncategorized No Comments

Bwana Yesu asifiwe ndugu katika Kristo Yesu.

Korbani ni neno limeonekana mara moja tu!, katika Biblia.(Marko 7:11) sasa maana yake ni nini?.

Marko 7:8-13 

“8 Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.

 9 Akawaambia, Vema! Mwaikataa amri ya Mungu mpate kuyashika mapokeo yenu. 

10 Maana Musa alisema, Waheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye babaye au mamaye kufa na afe. 

11 Bali ninyi husema, Mtu akimwambia babaye au mamaye, NI KORBANI, yaani, wakfu, kitu changu cho chote kikupasacho kufaidiwa nacho, huwa basi; 

12 wala hammruhusu baada ya hayo kumtendea neno babaye au mamaye; 

13 huku mkilitangua neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyopokeana; tena mwafanya mambo mengi yaliyo sawasawa na hayo.

Ukisoma huo Mstari wa 11 utaona neno hili limetolewa ufafanuzi “NI KORBANI, yaani, wakfu,”  hivyo.

Korbani. ni kitu chochote kilichotolewa wakfu kwa Bwana, kama vile dhabihu,(sadaka ya kuteketezwa),sadaka ya shukrani kwa Bwana,au matoleo yoyote yale yahusuyo kumtolea Bwana.

Hivyo Bwana Yesu aliwaambia maneno hayo Mafarisayo na Waandishi baada ya kumuuliza swali kwa nini wanafunzi wake wanakula bila kunawa mikono mpaka kwemye viwiko nk Yesu akawajibu wao wanaiarifu Sheria ya Bwana(Nullify)yaani kuibatilisha sheria ya Mungu.

Ambapo Mungu aliagiza watu wawaheshimu Baba zao na Mama zao. Si kuwaheshimu kwa kuwasalimia tu au kuwatii tu wanapowaagiza kufanya jambo fulani la!, bali ilikuwa ni zaidi ya hapo ilikuwa ikijuisha katika kuwaheshimu wazazi na kuwahudumia pia Kifedha.

Lakini Mafarisayo na Waandishi wao walikuwa wakiipotoa sheria hii na kusema kitu akishakiweka wakfu kwa Bwana hata kama mzazi wake anaumwa na inahitajika Fedha kwa ajiri ya matibabu kama Fedha akishaiweka wakfu haruhusiwi kubadili mawazo yake hata mzazi afe wala haitakuwq dhambi.

Hata wazazi wakiwa kwenye hali ngumu kimaisha na wanahitaji msaada wa watoto wao wawasaidiee walikuwa wakiwaambia hata usipowahudumia ukakiweka mbele za Bwana si dhambi. Hivyo ikapelekea jamii kubwa sana kuishi katika umasikini wazazi kukosa mahitaji ya msingi wakiwauliza watoto wao mbona huleti chakula nyumbani au hautusaidii wazazi wako? Jibu wanalokutana nalo nimekiweka wakfu kwa Bwana na hawawezi kuwafanya lolote wanaendelea kuwa wahitaji wasioweza hata kumudu chakula cha siku moja.

Jambo ambalo Mungu hakuagiza iwe hivyo kabisa.

Nini tunqjifunza juu ya jambo hili.

Biblia/Neno la Mungu limeagiza tuwahudumie watu wa nyumbani mwetu yaani ndugu zetu. Haijahalalisha ama kukimbia majukumu yetu kama vijana kuwahudumia wazee/ndugu zetu biblia inasema mtu asiehudumia jamaa za nyumbani mwake huyo ni mbaya kuliko hata mtu asieamini.

1 Timotheo 5:8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”

Lakini pia Biblia haijaagiza tuhudumie tu ndugu zetu peke bali pia na katika kumtolea Mungu maana ni sehemu ya ibada na kupeleka injili mbele maana injili pia inahitaji fedha ili watumishi wa Mungu wapeleke injili sehemu mbali mbali kuokoa roho za watu kama kanisa la kwanza lilivyofanya kutoa mali zao kwa ajili ya kuhudumiana lakini si hivyo tu bali kile kinachopatikana kinaenda kusaidia kupeleka injili mbele zaidi.

Hivyo usikwepe kutoa sadaka kanisani, kuwasaidia masikini,kuhudumia ndugu zako vifanye kila kimoja kitimilize wala hutapungukiwa Mungu atazidi kukuzidishia zaidi maana kila sehemu unayofanya hivyo ina baraka zake.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *