NINI MAANA YA TOBA?

Maswali ya Biblia No Comments

Toba ni neno lenye maana ya KUTUBU , unapofanya toba Moja kwa moja unaonekana umetubu,na ndo mana utaona neno kutubu lina maana ya kugeuka, unageuka Katika njia uliyokuwa ukiiendea..kwa mfano unapouendea mwenendo ambao sio mwema na kufikia hatua ya kugeuka Katika njia hiyo basi hapo unaonekana umetubu, au umefanya toba..

Kulingana na Maaandiko, mtu aliyeamua kugeuka na kuacha dhambi na kukaa mbali na mambo maovu Katika ulimwengu huu na kuomba msamaha kwa Mungu wake, mtu huyu anakuwa ameomba TOBA, kwa kuwa hi ndiyo hatua ya kwanza kabisa ya kuanza kukaa karibu na Mungu, Hakuna njia nyingine tofauti..

Ndo mana tunaona injili ya Yohana mbatizaji, aliye mtengenezea Bwana njia ilianza na Toba, na kuja kwa Bwana Yesu injili yake ilianza hivyo hivyo..

Yohana 3:1  “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,

2  TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Mathayo 4:17 “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, TUBUNI; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia”.

Kulimaanisha kuwa imefika kipindi cha watu kugeuka Katika njia zao mbaya, wageuke Katika maisha ya uzinzi, Maisha ya magomvi na matukano, maisha ya dhambi na uovu usiokwisha kwasababu siku ya mwisho watu wayatendao hayo hawataingia Mbinguni….

Ijapokuwa sio kutubu tu kuna kupa uhalali wote bali ni KUZAA MATUNDA YANAYOPATIKANA NA TOBA, kuanzia wakati huo unaanza kujichunga na kuishi maisha Matakatifu ili usirudie tena mambo maovu kamwe…

Luka 3:8 “Basi, toeni matunda yapatanayo na toba; wala msianze kusema mioyoni mwenu, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba katika mawe haya Mungu aweza kumwinulia Ibrahimu watoto

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *