UUNGU NI NINI?

  Maswali ya Biblia

2 Petro 1:3  Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe

4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

Ni ile hali ya kutaka kuwa kama Mungu au kufanana na Mungu inafahamika kama Uungu..

Mtu yeyote anayetenda vitendo viovu, ni muuaji, ni mzinzi, mtukakanaji, anafanya ushoga, mchawi, tunasema anafanya vitendo vya ushetani, kwasababu anatenda kazi za shetani..

Uungu ni kufanya kazi za KiMungu ndani yako na kuanza kuwa na sifa za Mungu, na tabia hizi za KiMungu si kila mtu anauwezo wa kuwa nazo bali ni wale walimpokea Kristo mioyoni mwao….

Tuangalie baadhi ya tabia za kiungu..

1. Uzima wa milele:

Biblia inasema karama ya Mungu ni uzima wa milele,na ndo kitu Yesu Kristo alichokileta kwa watu wake ulimwenguni, kwasababu tabia ya asili ya Mwanadamu hana uzima wa milele ndani yake, lakini aliyezaliwa mara ya pili anaishi milele kwasababu Uungu upo ndani yake..

Yohana 10:34  “Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu?”

Ukiwa ndani ya Yesu Kristo hakikisho hili la uzima wa milele linakuwa ndani yako, mtu mwovu hana uzima wa milele..

2. Matunda ya Roho..

Unapokuwa mwana wa Mungu lazima kuna tabia za Roho zitaanza kuonekana ndani yako, mfano, fadhili, Upendo, wema n.k…

Wagalatia 5:22-25

[22]Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,

[23]upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.

[24]Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.

[25]Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.

Sasa mambo kama hayo huwezi ukayaona yanatokea kwa mtu aliye nje ya Kristo kwasababu mwisho wa siku atachoka na kuonekana kuwa ni unafki tu, kwasababu havitoki moyoni mwake..

3. KUSHINDA DHAMBI:

Aliye na tabii ya uungu ndani yake anakuwa mwepesi na mwenye uwezo wa kushinda ulimwengu na mambo yaliyo ndani yake maovu, kwasababu tayari Kristo aliushinda ulimwengu..

1 Yohana 3:9

[9]Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

Dhambi inakuwa haina nguvu ndani yake, inafikia hatua unajiuliza tunawezaje kuishi maisha mbali na dhambi (1Petro 4:4).. imewezekana kwasababu nguvu za ki-Ungu zipo ndani yetu

Vifungu vinavyoelezea Uungu, Matendo 17:29, Warumi 1:20).

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT