SHINIKIZO NI NINI KIBIBLIA?

  Maswali ya Biblia

Shinikizo ni sehemu ya shimo au kisima kilichotengenezwa Mahususi kwa ajili ya kukamulia zabibu…Jinsi zabibu zinavyokamuliwa leo ni tofauti na kipindi cha zamani, kwa kipindi cha sasa tunaona ni mashine ndizo zinazotumika kukamua juisi yake..

Na walichokuwa wanakifanya baada ya kuchimba na kutengeneza kisima hicho , waliziweka zabibu ndani ya kisima na kisha wanaume huingia ndani yake na kuanza kuzikanyaga kanyaga wakishikilia kamba juu ili wapate uwiano mzuri , Kwa pembeni ya kisima hutengeneza kimfereji ambacho kinaelekeza juisi yote ya zabibu kwenye kisima kingine kidogo, ambacho ndani ya kijisima hichi huichota juisi ya zabibu ikiwa safi kwa Matumizi mbalimbali…

Tusome baadhi ya vifungu

Mathayo 21:33 “Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri..

34 Wakati wa matunda ulipokuwa karibu, akawatuma watumwa wake kwa wale wakulima, wapokee matunda yake”.

Hagai 2:16 “katika wakati huo wote, mtu alipofikia chungu ya vipimo ishirini, palikuwa na vipimo kumi tu; na mtu alipofikia shinikizo apate kuteka divai ya vyombo hamsini, palikuwa na divai ya vyombo ishirini tu.

Soma pia, Isaya 5:2, Hagai 2:16, Waamuzi 7:25, Nehemia 13:15, Ayubu 24:11, Isaya 63:3

NENO HILI LINAFUNUA NINI ROHONI?

Tukisoma kitabu cha Ufunuo tunaona Bwana Yesu Kristo anajionyesha kuwa yeye ndiye atakayekanyaga shinikizo la ghadhabu ya Mungu siku ile ya Mwisho

Ufunuo 19:15 “Na upanga mkali hutoka kinywani mwake ili awapige mataifa kwa huo. Naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, naye anakanyaga shinikizo la mvinyo ya ghadhabu ya hasira ya Mungu Mwenyezi”.

Kwa lugha nyepesi ni kuwa Bwana Yesu ndiye atakayeitekeleza hasira ya Mungu kwa watu wote waovu watakaokuwa ulimwenguni, na wakati huo unyakuo utakuwa umepita , Mataifa yote yatalia na kumuombolezea siku ya kurudi kwake , kutakuwa na mambo ya kutisha sana, mpaka biblia inatuambia watu watatamani mpka milima iwaangukie wajiepushe na ghababu ya Mungu, lakini haitawezekana mpka washiriki mapigo hayo, Ni Yesu atakayeitekeleza ghadhabu hiyo.. watu watakufa na damu nyingi kumwagika sana..

Ufunuo 14:19 “Malaika yule akautupa mundu wake hata nchi, akauchuma mzabibu wa nchi, akazitupa zabibu katika shinikizo hilo kubwa la ghadhabu ya Mungu.

20 Shinikizo lile likakanyagwa nje ya mji, damu ikatoka katika shinikizo mpaka kwenye hatamu za farasi, kama mwendo wa maili mia mbili”.

SIO KIPINDI CHA KUKITAMANI ,Siku ya Bwana inatisha sana

Ufunuo 16:19 “Na mji ule mkuu ukagawanyikana mafungu matatu, na miji ya mataifa ikaanguka; na Babeli ule mkuu ukakumbukwa mbele za Mungu, KUPEWA KIKOMBE CHA MVINYO YA GHADHABU YA HASIRA YAKE.

20 Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.

21 Na mvua ya mawe kubwa sana, ya mawe mazito kama talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya wanadamu. Wanadamu wakamtukana Mungu kwa sababu ya lile pigo la mvua ya mawe; kwa maana pigo lake ni kubwa mno”.

Hivyo ndugu yangu tujihakikishe tupo upande salama, Ni Kwa kumpa YESU KRISTO maisha yetu , ni mda Mfupi sana tumebakiwa nayo, tusiichezee hii neema tunayoiona upo wakati itaondolewa….

Shalom,

Pia unaweza kujiunga na channel yetu ya Mafundisho zaidi, NURU YA UPENDO” Kwa kubofya hapa>> WhatsApp: https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Washirikishe wengine habari hizi njema Kwa kushea, au wasiliana nasi kwa namba hii 255789001312,255693036618

LEAVE A COMMENT