Marko 12:26 “Na kwa habari ya wafu ya kwamba wafufuliwa, hamjasoma katika kitabu cha Musa, SURA YA KIJITI, jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?”
jibu: Sura ya kijiti iliyozungumziwa hapo si sura ya mti yaani umbile la mti, au sura ambayo ina pia mdomo na macho hapana, bali hapo mwandishi alimaanisha “mlango wa”
mfano labda, tukitaka kusoma habari fulani katika biblia, kiongozi anaweza sema fungua Mathayo mlango wa pili mstari wa nane, hapo ni sawa na kusema fungua Mathayo sura ya pili mstari nane, kwahiyo hivyo vitu vipo sawa
au tunaweza kusema habari za ubatizo zinapatikana kaka kitabu cha matendo sura ya pili
Kwahiyo hata hapo mtume paulo alipokuwa anasema habari hiyo ya “sura ya kijiti” alikuwa ana maanisha sura ile ya kwenye maandiko pale Mungu alivyozungumza na Musa kupitia kile kijiti kilichokuwa kinawaka moto lakini hakiteketei, kwahiyo hapa paulo hakuzungumzi kipande cha mti bali alimaanisha mlango , kwa kunukuu habari hiyo ya Musa
tunaipata mahali hapa
Kutoka 3:1 “Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
2 Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
3 Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu KIJITI HIKI HAKITEKETEI.
4 Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka KATIKATI YA KILE KIJITI, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
5 Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
6 Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.
7 Bwana akasema, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri”
Ni Nini tunajifunza hapa ukiendelee katika hiyo habari aliyoiandika paulo anasema “jinsi Mungu alivyomwambia, akisema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?” hapo alikuwa anaonyesha kuwa Mungu ni Mungu wa walio hai, Sasa unaweza jiuliza kivipi awe hai kwa watu walikufa mfano Ibrahimu, Isaka na Yakobo, maandiko yanatueleza jambo hili
Yohana 11:25 “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”
Kwahiyo igawa hao kina Ibrahimu, Isaka na Yakobo wamekuja lakini wapo hai huko walio kwa sababu katika maisha yako walimwamini Mungu; Nasi pia tukimwamini Bwana Yesu katika maisha yetu hata tutakapo kufa tutaendele kuishi Kristo Yesu mwenyewe amesema kuwa “Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”
Je umemwamini Yesu maishani mwako, ikiwa tayari basi endelea kukaza mwende Kwa kuishi maisha yapasayo Toba, na ikiwa bado basi fanya maamuzi mapema maana hujui ya kesho yatakayo tokea ili hata utakapo kuwa Leo uwe na tumaini la kuishi.
Waebrania 11:16 “Lakini sasa waitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. KWA HIYO MUNGU HAONI HAYA KUITWA MUNGU WAO; maana amewatengenezea mji”.
shalom
Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea
Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.
Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1
Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618
Bwana akubariki.