Wapunga Pepo ni watu gani katika Biblia?.

  Maswali ya Biblia

Shalom!, Nakusalimu katika jina la Mwokozi wetu Yesu Kristo.

Wapunga Pepo kama tunavyosoma katika maandiko Matendo ya Mitume 19:13. Biblia inataja ni wana wa Skewa, Sasa maana nyingine ya kupunga Pepo ni KUFUKUZA PEPO.

Sasa zipo namna mbali mbali za kufukuza pepo/kupunga Pepo.

Moja ni kupitia Watumishi wa Mungu na nyingine ni kutumia Waganga na Wachawi(ushirikina) sasa njia iliyo sahihi na ya kumfungua mtu kweli kweli ni kupitia Watumishi wa Mungu wanaofanya kazi hiyo kwa mamlaka ya jina la Yesu!.

Waganga/wachawi kwa kawaida hawawezi kutoa pepo yaani pepo kumtoa pepo mwingine ni jambo lisilowezekana maana ufalme wa giza utafitinika!.

Sasa unaweza ukawa umeshaenda kwa waganga huenda wewe mwenyewe ama ulishaenda na ndugu yako akatolewe Pepo linalomsumbua kwenda kuaguliwa kule wanaita MAJINI sasa pale kweli unapoona ndugu yako ama wewe umepona lile pepo lililokuwa ndani yake/yako limetoka hapo linakuwa halijatoka lakini kuna jambo linalofanyika hapo…

Jambo linalofanyika ni wewe/yeye kupewa pepo lenye nguvu zaidi kushinda lile la Mwanzo hivyo linafunika lile lililokuwepo na linakuwa limezima tu na Jambo lile ulililokuwa linakusumbua linaonekana kama limeisha lakini sivyo!.

Kama mwanzoni labda lilikuwa linakusababishia kifafa lile la Mwanzo litakapo kuja lile lingine Litaleta ugonjwa mwingine baadae huenda ukaanza kupalalalyse nk. Hivyo kwenda kwa waganga kuaguliwa si kwamba unapona bali unaongeza tatizo lingine!.

Maana ufalme hauwezi kufitinika yaani Shetani amtoe Shetani mwenzake haiwezekani ndio maana Bwana watu Yesu Kristo akasema….

Mathayo 12:26 “Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?”.

Je!? Umeokoka au bado unaendelea kwenda kwa waganga na wachawi kuaguliwa? Jua ndoo unavyozidi kujiweka katika vifungo na maagano mengi. Okoka sasa mpe Bwana Yesu Kristo maisha yako uwe salama. Maana ukishamwamini Yesu uchawi,uganga, mapepo, majini nk yanakuwa hayana nguvu juu yako. Uhai wako unafichwa katika Kristo Yesu.

Bado unayo nafasi lakini haitadumu milele
Tubu sasa mgeukie Bwana Yesu upate msamaha wa dhambi upate na uzima wa milele pia.

Ubarikiwe sana!,
MARANATHA

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

LEAVE A COMMENT