Nini maana ya Masheki ?

Maswali ya Biblia No Comments

Bwana Yesu apewe sifa!, karibu katika kujifunza Neno la Mungu.

Je neno mesheki linamaanisha nini?
Neno hili tunalipata katika vifungu vifuatavyo (Zaburi 105:22,Ayubu 29:10,Zaburi 68:31). Sasa maana yake ni nini?.

Masheki Ni watu wenye hadhi kubwa(watu wenye uwezo na Mamlaka)ambao sauti zao zinasikika na kuogopwa wakiongea nchi yote ama jamii yote wanatega sikio kusikiliza ni nini wanasema!.

Kwahiyo ni watu wenye heshima, na wana jina kubwa katika Jamii, katika Taifa/serikali au Dunia nzima wao huwa wanajulikana na kuogopwa.

Tunaliona hilo katika kitabu cha

Ayubu 29:9 “Wakuu wakanyamaa wasinene, Na kuweka mikono yao vinywani mwao;

10 Sauti yao masheki ilinyamaa, Na ndimi zao zilishikamana na makaakaa yao”.

Pia Soma.

Zaburi 68:31 “Masheki watakuja kutoka Misri, Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara”.

Tunasoma pia..

Zaburi 83:11 “Uwafanye wakuu wao kama Orebu na Zeebu, Na masheki yao wote kama Zeba na Zalmuna”.

Zaburi 105:22 “Awafunge masheki wake kama apendavyo, Na kuwafundisha wazee wake hekima”.

Sasa hata katika Ulimwengu unaokuja Kristo atakaporudi na kutawala pamoja watakatifu wake. (Masheki) yaani waliokombolewa ndio watakuwa na sauti kubwa, Majina Makubwa na hadhi kubwa milele yaani mimi na wewe(watakatifu tuliokombolewa).

Sisi sote tunaokaa katika dunia hii iliyopotoka na wale waliomwamini Kristo na kuvipiga vita vya imani hapo zamani na hata sasa wakashinda hao watakuwa ni Masheki katika ulimwengu unaokuja.. maana
Ahadi zake alizosema ni kweli na Neno lake ni kweli na ahadi hizo ni kama.

Ufunuo 2:26 “Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,

27 naye atawachunga kwa fimbo ya chuma, kama vyombo vya mfinyanzi vipondwavyo, kama mimi nami nilivyopokea kwa Baba yangu”.

Soma pia..

Ufunuo 3:12 “Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya”.

Ufunuo 3:21 “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

22 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa”.

Swali la kujiuliza Je! Uko miongoni mwa wale watakofanyika kuwa masheki katika ulimwengu unaokuja wa milele? Kubali kujitaabisha leo kwa ajili ya Kristo jikane nafsi yako leo ili siku ile ufanyike kuwa Masheki milele.

Ubarikiwe sana.

Washirikishe na wengine habari hizi njema kwa kushea

Ikiwa utapenda kupata msaada wa kumpokea Yesu maishani mwako bure, Basi wasiliana nasi kwa namba uzionazo chini ya makala hii.

Pia kwa kupokea mafundisho ya kila siku kwa njia ya WHATSAPP, jiunge na channel yetu kwa kupofya link hii >> https://whatsapp.com/channel/0029VaBVhuA3WHTbKoz8jx1

Kwa Mawasiliano: +255789001312 au +255693036618

Bwana akubariki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *